LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 1, 2022

CHIFU MWAKATUMBULA WA WANYAKYUSA AKABIDHIWA IKULU YAKE LEO

Na Chriatopher Lissa, UPL

Hatimaye Chifu wa kabila la Wanyakyusa Chifu Edwin Mwakatumbula leo amekabidhiwa Ikulu yake ya Kichifu na kiongozi wa machifu wadogo wa kabila hilo.


Akizungumza katika tukio hilo la kihistoria, Chief Edwin amesema kuwa imekuwa siku ya baraka kwenye himaya hiyo, kwa yeye kukabidhiwa Ikulu hiyo iliyojengwa Mwaka 1900.


Aidha amesema kuwa kazi aliyokabidhiwa na machifu wadogo wa kabila hilo ataendelea kuifanya kwa kuzingatia mila na desturi za kabila hilo maarufu nchini.


Amesema kuwa aliporithi uchifu wa kabila hilo kutoka kwa marehemu Chifu Daudi B Mwakatumbula miaka 10 iliyopita amejitahidi kuendeleza mila za kabila hizo huku akidumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wanyakyusa wote nchini.


Chief Edwin ni miongoni mwa watoto 72 wa marehemu Chief Bentamanile Mwakatumbula wa kabila ilo ambaye alifariki dunia mwaka 1955 huku akicha wake 52 .


Vitabu vya kihistoria vya kabila la Wanyakyusa vinamtambua Chifu Bentamanile Mwakatumbula kwa mageuzi makubwa ya kiutawala aliyoyafanya wakati wa utawala wake wa miaka 45.


Katika kuthibitisha hilo, Alikuwa Chifu pekee kutoka Tanganyika aliyekabidhiwa Cheti cha heshima kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza.


Wakati wa utawala wake, alihesabiwa miongoni mwa machifu wa kimila waliokuwa mstari wa mbele kuipambania nchi uhuru, huku Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius K Nyerere akisema kuwa kazi kubwa waliyoifanya kipindi hiko katika Mikoa ya kanda za juu kusini hususani mkoa wa Mbeya zilikuwa za kutukuka na kurahisisha kuiunganisha nchi.


KIONGOZI wa Machifu wadogo wa kabila la wanyakyusa Salim Mwakalinga (kulia) akimkabidhi ngome ya kichifu  Chifu wa Mkuu wa Wanyakyusa Chifu Edwin Mwakatumbula ( Aliyevaa Suti Nyeusi),Ikulu 'ngome ya kichifu' hiyo inayoitwa London ipo katika Kijiji  cha Masoko, Wilayani Rungwa Mkoa wa Mbeya,baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa,Jana.(Picha na Christopher Lissa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages