LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 23, 2022

WAZIRI MASAUNI AONGOZA MAADHIMISHO YA 92 YA SIKU YA TAIFA LA SAUDIA, JIJINI DAR ES SALAAM

Na Felix Mwagara, MoHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameipongeza Serikali ya Saudia Arabia kwa maadhimisho ya siku ya 92 ya Taifa hilo la Kifalme yaliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam, jana Septemba 22, 2022.

Waziri Masauni ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe ya maadhimisho hayo, alisema Serikali ya Tanzania inatoa pongezi hizo kwa taifa hilo na pia kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi hiki cha Uongozi wa Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa pongezi kwa maadhimisho haya na pia inaishukuru Serikali ya Saudia kwa ushirikiano wa muda mrefu uliodumishwa kupitia sekta za kilimo, afya na maji na imeahidi kuendeleza ushirikiano huo kwa faida ya nchi zote mbili,” alisema Masauni.

Waziri Masauni kupitia maadhimisho hayo amewakaribisha wawekezaji kutoka Saudia Arabia kuja nchini kuwekeza na pia kwa waliopo waendelee kuongeza nguvu zaidi ya kuwekeza kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyoboreshwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Balozi wa Saudi Arabia nchini, Balozi Abdullah Ali Alsheryan, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano waliokuwa nao kwa Taifa hilo na ameahidi wataendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandishi Masauni Hamad Masauni akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya 92 ya Taifa hilo la Kifalme yaliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam, jana Septemba 22, 2022.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages