LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 10, 2022

MWILI WA PRINCE PHILIP KUPELEKWA ATAKAKOZIKWA MALIKIA ELIZABETH II

Na Polycarp Mdemu 

Kutokana na Kifo cha Malkia Elizabeth II sasa mwili wa Mumewe Prince Phillip  utaondolewa pale ulipohifadhiwa tangu kifo chake mwaka wa 2021, na kupelekwa mahali ambako mwili wa Malkia utazikwa.


Mnamo 2021 mwili wa Philip uliteremshwa futi 15 ndani ya Jumba lenye umri wa miaka 200 chini ya St George's Chapel huko Windsor Castle ambako umehifadhiwa mpaka leo.


Kwa mpangilio wa utangulizi, mwili wa Philip haukuweza kupelekwa Vault kabla ya Malkia ambaye ndiye aliandaliwa  Kwa hiyo mwili wake ulipaswa kuwekwa mahali fulani kwa muda.


Hapa palikuwa tu mahali pa kupumzika au tuseme kuhifadhiwa kwa muda kusubiri kifo cha Malkia (Mkewe) siku kitapotokea.  Kijadi Mme wa Malkia au Mke wa Mfalme anatakiwa kutanguliwa Hatua mbili mbele ya Mfalme/Malkia.


Vault katika kanisa la ukumbusho la Mfalme George VI lilikuwa limetengwa kama mahali pa mwisho pa kupumzika kwa Malkia.  Ilijengwa mnamo mwaka 1810 na 1814, na inahifadhi mabaki ya Baba wa Malkia George VI, Mama wa Malkia na Dadaye Princess Margaret.


Sasa kwa kuwa Malkia amekufa, Philip pia atahamishiwa kwenye jumba la kumbukumbu la King George VI ili kulala pamoja na mke wake wa miaka 73, ili waweze kuunganishwa katika kifo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages