Na Bashir Nkoromo, Kigamboni
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigamboni, Dar es Salaam, Stanleya Mkandawile amewahimiza Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Wilayani humo kuyasema kwa Wananchi mambo ya maendeleo ambayo Serikali ya Awamu ya Sita chini Rais Samia Suluhu Hassan imeyafanya.
Mkandawile amesema hayo katika Kikao cha Baraza la dharula la Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kigamboni, kilichofanyika katika Ofisi ya CCM wilaya hiyo jana, kwa ajili ya kuteua Wajumbe 7 wa Baraza la Utekelezaji la muda, linakaloteua wagombea, kutokana na Wajumbe saba wote kuomba tena kugombea.
"Baada ya Uchaguzi tutaandaa semina kwa lengo la kuwawezesha viongozi wapya wa Jumuiya ya Wazazi kujua majumu yao kama viongozi wa Jumuia, maana Jumuiya hii ni Jumuiya yenye kazi muda wote tofauti na Jumuiya zingine za Chama.
Kazi za jumuia hii ambazo hazina muda ni Elimu, Malezi, Mazingira, Utamaduni, na kuisimamia na kuisemea Serikali kwa Wananchi. Katika kuismamia Serikali mnaitisha vikao na kuzungumza na watendaji ili wawape mrejesho wa utekelezaji wa Ilani, lakini kuisemea Serikali mnazungumza na wanannchi", akasema Mkandawile.
"Na ili kuisemea serikali ni lazima muelewe iliyoyafanya hasa katika ngazi za Kata na wilaya mnayoongoza, na haya mnayapataje, ni kwa kufanya vikao na watendaji wa serikali katika ngazi hizo. Kwa mfano, katika Bajeti ya mwaka huu tunanunuliwa Kivuko kipya na pia zitajengwa Kilometa 41 za Barabara kwa kiwango cha lami, hii ikiwa na maana kwamba barabara zote Wilaya ya Kigamboni zitakuwa za lakimi.
Hata kama makubwa hamyajui, lakini hata haya yanayofanywa na Serikali hapa Wilaya ya Kigamboni nayo hamyajui? Basi yasemeni kwa wananchi maana hili ninyi viongozi wa Jumuiya ya Wazazi linawahusu, ni moja ya majukumu ya Jumuiya hii", akasema Mkandawile.
Aidha Mkandawile amesema jumuku lingine linaoihusu Jumuiya ya Wazazi ni viongozi wa Jumuia kutokuwa sehemu ya wanaoilalamikia mitaani Serikali, badala yake kama kuna jambo haliko sawa waitishe kikao kujadili changamoto iliyopo ili kupata ufumbuzi na kama ni nje ya uwezo wao waishauri serikali nini kifanyike.
Pia amesema, viongozi wa Jumuiya hawapaswi kushiriki kuwasema vibaya mitaani Viongozi au Watendaji wa Serikali wanaoonekana wanaenda ndivyo-sivyo, badala yake wanatakiwa wawaite na kuwaelekeza ili wabadilike na kama imeshindikana wachukuliwe hatua za juu zaidi.
"Jambo lingine ni kwamba Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi hampaswi kuungana na wananchi kulalamikia mitaani miongozi au Watendaji, mjue kwamba Kiongozi au Mtendaji wa Serikali akionekana mbaya maana yake Chama ndiyo kibaya, ikifika siku ya uchaguzi hata Chama kikiweka mgombea mwingine bado kitaelemewa na ubaya wa yule kiongozi au Mtendaji mliyekuwa mnasema mitaani.
Kwa hiyo kinachotakiwa, anapotokea Kiongozi au mtendaji kama Diwani au Mbunge wa CCM anafanya ndivyo-sivyo, mwiteni katika vikao maalum, mwelezeni kwa uwazi kisha mkanyeni, na kama habadiliki chukueni mfikisheni ngazi za juu kwa hatua zaidi.", akasema Mkandawile.
Your Ad Spot
Sep 2, 2022
Home
featured
siasa
MKANDAWILE AHIMIZA JUMUIA YA WAZAZI KUYASEMA KWA WANANCHI MAKUBWA YANAYOFANYWA NA RAIS SAMIA KIGAMBONI
MKANDAWILE AHIMIZA JUMUIA YA WAZAZI KUYASEMA KWA WANANCHI MAKUBWA YANAYOFANYWA NA RAIS SAMIA KIGAMBONI
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇