KIJANA Innocent Chengula anayeishi jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kujifanya yeye ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abass na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Mwandamizi Mwanaamina Kombakono akisaidiana na wakili wa serikali Batlida Mushi imedai Chengula anakabiliwa na jumla ya mashtaka sita
Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Yusto Ruboroga na imedaiwa kuwa, Julai 26 mwaka huu katika sehemu tofauti ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mshitakiwa huyo kupitia Kompyuta yake aina ya Infinix alijitambulisha kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete kuwa yeye ni Dkt Hassan Abass wakati akijia si kweli.
Imeendelea kudaiwa kuwa, Julai 8, 2022 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mshitakiwa huyo alijitĂ mbulisha kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Wallace Karia ,kuwa yeye ni Dkt Hassan Abass huki akijua kuwa siyo kweli.
Pia imedaiwa, Julai 26 mwaka huu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mshitakiwa Chengula kwa njia ya udanganyifu alijipatia shilingi milioni nne kutoka kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete,baada ya kujitambulisha kuwa yeye ni Dkt Hassan Abass.
Aidha, kati ya Juni hadi Agosti mwaka huu mshtakiwa huyo alitumia laini za simu za watu wengine ambao ni Asha Shabani Nuru Salum Maulid na Deogratius Michael Kimario bila kutoa taarifa kwa mamlaka husika.
Hata hivyo mashtakiwa amekana kutenda kosa hilo ma amerudishwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya sh. Milioni kumi
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe nyingine ya kuja kumsomea mshtakiwa hoja za awali ambapo imepangwa Oktoba 10 mwaka huu.
Kijana Innocent Chengula akirudishwa mahabusu mara baada ya kusomewa kesi yake inayomkabili ya kujitambulisha kwa majina yasiyo kwake na kutapeli sh. Milioni nne, kesi hiyo imesomwa leo Septemba 26, 2022 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇