Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Njombe, Fulgence Kanuti ameupongeza uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABIT) kwa kazi nzuri ya urasimishaji ardhi na viwanja wanaoifanya mkoani Njombe na kwamba huo ni msaada mkubwa katika sekta ya ardhi.
Ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya utoaji hatimiliki za viwanja kwa wakazi wa Tandala na Ikonda wilayani Makete Septemba 25, 2022.
Kazi zingine zilizofanywa na MKURABITA ni uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa jengo la masjala katika Kijiji cha Malembuli, Kata ya Mang'oto siku hiyo Septemba 25, 2022 na uzinduzi wa jengo la masjala katika Kijiji cha Mwakauta wilayani Makete.Pia uongozi wa MKURABITA ulifanya ziara ya ufuatiliaji wa kazi walizozifanya awali za upimaji viwanja katika Halmashauri ya Mji Makambako.
Wananchi wakishangilia wakati wa hafla hiyo.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Makete, Alex Ngailo akimkabidhi hatimiliki ya kiwanja mmoja wa wakazi wa Ikonda wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa MKURABITA, Dkt Seraphia Mugembe (kulia) akimpongeza mmoja wa wazee wa Tandala kwa kupata hatimiliki ya kiwanja.
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi waliopatiwa hatimiliki za viwanja.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Kanuti akitoa pongezi hizo...
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇