LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 22, 2022

UVCCM KIGAMBONI 'WALIVYOWASHA MOTO' JUZI, KONGAMANO LA KUHAMASISHA SENSA ITAKAYOFANYIKA KESHO AGOSTI 23, DC NYANGASA AWAPONGEZA

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Fatma Almas Nyangasa akiongoza matembezi ya Kongamano la kuhamasisha Wananchi kujitokeza kuhesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika kesho, Agosti 23, 2022. Matembezi ambayo yalianzia njiapanda Vijibweni na kumalizikia katika Ukumbi wa Peace Park kwa ajili ya Kongamano yalifanyika juzi. Kulia kwa DC Nyangasa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya hiyo ya Kigamboni Komredi Mponela Mathei. Kushoto kwa DC huyo ni Katibu Mwenezi wa CCM pia Wilaya hiyo Ndugu Pazi.
Matembezi yakiendelea mtaa kwa mtaa👇
Matembezi yakiendelea
Matembezi yakiendelea huku yakiongozwa na bodaboda wenye hamasa ya kutosha.
Bodaboda wakiwasili kwa amshaamsha kwenye Ukumbi wa Peace Park
DC Nyangasa na Viongozi wa  UVCCM Kigamboni wakiwasili Viwanja vya Ukumbi wa Peace Park
Matembezi yakifika ukumbi wa Peace Park
DC Nyangasa akizungumza kidogo na Mwenyekiti wa UVCCM Kigamboni  Komredi Mponela Mathei nje ya Ukumbi wa Peace Park
"Yaani hapa kila kitu kipo Sawa", Mwenyekiti wa UVCCM Kigamboni Komred Mathei akiwambia DC Nyangasa
Vijana kutoka kata zote tisa za Wilaya ya Kigamboni wakiwa wamesheheni ukumbini.
Katibu wa Hamasa UVCCM Kigamboni Komredi Kareem akichangamsha ukumbi.
Katibu wa UVCCM Kigamboni Amina Kizigo akifanya utambulisho kwa hamasa ya kipekee
Vijana wakamshangilia
Vijana wakiimba utenzi
Vijana wa hamasa wa UVCCM Kigamboni wakachangamsha ukumbi wa kucheza 'maghirighiri' ya kisasa
Vijana wakipagawa ukumbini.
Katibu wa UVCCM Ilala Jesca Msengi akiwapa salam Vijana wa UVCCM Kigamboni.
Vijana wakimshangilia
Ukumbi ukawaka kwa nderemo za vijana
Katibu wa UVCCM Temeke Ndugu Nehemia akasimama kusalimia
Katibu Mwenezi wa CCM Kigamboni Ndugu Pazi naye akasimama kutoa neno
Katibu wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Msuya akizungumza.
Katibu wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Msuya akiendelea kuzungumza.
Vijana wakimsikiliza huku wamekaa kwa 'kujiachia' kwa raha zao.
Katibu wa UVCCM- Seneti mkoa wa Dar es Salaam Geofrey Kiliba akizungumza
Mwenyekiti wa UVCCM Kigamboni akizungumza
Katibu wa UVCCM Kigamboni akiwa na Makatibu wenzake wa UVCCM kutoka Ilala, Temeke na Katibu wa UVCCM Ubungo Nehemia Philemon.
Vijana Ukumbini
Mwenyekiti wa UVCCM Kigamboni akionyesha cheti kati ya vyeti ambavyo DC Nyangasa aliwakabidhi Vijana wote wa UVCCM Kigamboni kwa kutambua mchango wao katika shughuli mbalimbali za Chama na Serikali ikiwemo mapokezi ya Mwenge yaliyofanyika hivi karibuni katika Wilaya hiyo.
Mwenyekiti wa UVCCM Kigamboni akiendelea kuzungumza
DC Nyangasa akimkabidhi cheti Diwani wa Vijibweni  Zacharia Mkundi cha kutambua mchango wake kwa shughuli za UVCCM, CCM na Serikali wilayani Kigamboni.
DC Nyangasa akimbidhi cheti mmoja kati ya Vijana wa UVCCM Kigamboni.
Vijana wakiserebuka ukumbini. Kisha ikafuatia zamu ya Keki maalum ya UVCCM Kigamboni kuhamasisha Sensa👇

DC Nyangasa akikabidhiwa keki hiyo
Kisa akaikata keki hiyo. Kisha ikafuatiwa DC Nyangasa kupewa tuzo ya ngao kutoka kwa UVCCM Kigamboni kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuwalea vijana na uchapakazi wake wa kumwakilisha vema Rais Samia Suluhu Hassan katika Wilaya ya Kigamboni.
Mwenyekiti wa UVCCM Kigamboni akionyesha ngao hiyo katika ya kuikabidhi kwa DC Nyangasa. Kushoto ni Ndugu Kizigo akifurahi
Mwenyekiti wa UVCCM Kigamboni akakabidhi ngao hiyo kwa DC Nyangasa
DC Nyangasa akionyesha ngao hiyo huku akiifurahia

DC Nyangasa akasimama ili kuzungumza na vijana wa UVCCM Kigamboni.
Vijana wakalipuka kumshangilia ukumbini
DC Nyangasa akazungumza akisema "Hakika naupongeza Uongozi na Vijana wote wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) katika Wilaya hii, kwa kuwa mstari wa mbele kuiunga mkono Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha zoezi hili muhimu la Sensa ya Watu na Makazi. Hakika mmeonyesha mfano mzuri".
DC Nyangasa akiendelea kuzungumza.
Vijana wakimsikiliza kwa makini DC Nyangasa.
Vijana wakimsikiliza DC Nyangasa
Viojana wakimsikiliza DC Nyangasa huku wakiwa na bango lao
Diwani wa Kimbiji Ndugu Sanya akizungumza na kuahidi kutoa Sh. 50,000 hapo hapo kwa ajili ya UVCCM Vijibweni, Kulia ni Diwani wa Vijibweni  Ndugu Mkundi.
Diwani wa Vijibweni Ndugu Mkundi (kushoto), naye akizungumza na kuahidi kutoa papohapo sh. 50,000 kwa Vijana kutoka Kata zote tisa za Wilaya ya Kigamboni.
Kisha akakabidhi 'mpunga' huo.
DC Nyangasa akaanza kukabidhi fedha hizo Kata baada ya Kata
DC Nyangasa aakizindikizwa na Mwenyekiti wa UVCCM Kigamboni Komrade Mponela mwishoni mwa shughuli hiyo.
DC Nyangasa aakiagana na katibu wa UVCCM Dar es Salaam Komredi Msuya
DC Nyangasa akiaagana na Diwani wa  Komredi Mkundi. ©August 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages