Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa Bahati Henerico akitoa taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo
Kyerwa.
Akizungumzia tukio hilo kupitia kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bahati Henerico amesema vifaa hivyo vimekamatwa wakati wa zoezi la udhibiti wa magendo ambapo wamefanikiwa kukamata kahawa iliyokuwa katika harakati za kutoroshwa kwenda nje ya nchi pamoja na kumilikiwa kinyume na sheria katika mazingira mbali mbali.
Kufuatia hali hiyo mwenyekiti huyo amemuomba mgeni rasmi katika kikao hicho Bwana, Musa Jumanne kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo kutoa maelekezo ya serikali kwa wananchi ambao dira ya siyo ya kuuza kahawa hapa nchini bali mpango wao ni kuipeleka nje ya nchi.
Aidha kupitia kikao hicho Bwana Jumanne amewaomba wananchi wa wilaya hiyo walio na kahawa kuweka njia nzuri kuipeleka katika vyama vya msingi AMCOS huku akiahidi kuanza kwa msako mkali wa kujua ni akina nani wana kahawa ili sheria ichukukue mkondo wake.
"Kikosi cha kudhibiti magendo kinaendelea kupambana na wale wanaomiliki kahawa majumbani na wale wanaowaza kuivusha kahawa nje ya nchi tutawakamata alisema Jumanne.
Naye mbunge wa jimbo la Kyerwa innocent Bilakwate amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutambua ili serikali iwaunge mkono katika shughuli za maendeleo mapato yanayopatikana ndiyo yanayosaidia miradi mbali mbali kwa wananchi.
Bilakwate amempongeza Rais Samia kwa kuhakikisha anaweka utaratibu mzuri wa kahawa kuuzwa kwa njia nzuri ambapo utaratibu huo umesaidia wakulima walionyonywa kunufaika na zao hilo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇