LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 6, 2022

STANLEY BETRAM ELIA: MWENYEKITI MPYA CCM KATA PANGANI KIBAHA

Kutoka kulia ni Stanley Betram Elia Mwenyekiti mpya wa CCM Kata Pangani aliyeshinda kwa kura 141. Kushoto kabisa ni Hashim Pumbuli (kura 50) na mwenye tai ni Msofe Msofe (kura 26).


Na Dismas Lyassa, Kibaha


MWANASIASA mkongwe Stanley Betram Elia ameibuka kidedea katika nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Pangani, Kibaha Mjini Mkoani Pwani.

 

Stanley ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mtakuja, mojawapo ya matawi 10 ya kata hiyo, amewahi pia kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Kata.

 

Baadhi ya wapiga kura walisikika wakisema wanaamini anaweza kusaidia kuimarisha chama na Serikali kwa ujumla katika kata hiyo kwa sababu tayari ana ufahamu na uzoefu wa kutosha.

 

“Jukumu lake ni kuimarisha chama kwa kushirikiana na viongozi pamoja na wanachama wengine, tunafikiri anaweza kutusaidia kwa sababu kama ni changamoto zinazoweza kutokea kwenye matawi, tayari amewahi kuwa kiongozi wa tawi anajua, pia kwenye Serikali ameshawahi hivyo anajua,” alisikika akisema mpiga kura mmoja.

 

Katika uchaguzi huo Stanley alipata kura 141 akifuatiwa na Hashim Pumbuli aliyepata kura 50, huku wa mwisho alikuwa Msofe Msofe aliyepata kura 20.

Aidha katika nafasi ya Ukatibu, ndugu Masudi aimshinda Said Liunde aliyekuwa akitetea nafasi hiyo, huku nafasi ya Mwenezi ikichukuliwa na James Mgaya.

 

“Uchaguzi kata Pangani umekwisha, sasa tuchape kazi, tupambane kuangalia na kutekeleza ilani” walisikika wakisema wapiga kura.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages