CCM Lumumba, Dar es Salaam
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesisitiza kwamba dhamira na azma ya Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan ya kuvifanyia maboresho ya kimfumo na kiteknolojia vyombo vya habari vya CCM haijapoa na imeanza kufanyiwa kazi.
Amesema leo la Mwenyekiti wa CCM Rais Samia kuvifanayia maboresho vyombo hivyo vya habari vya CCM ni kuhakikisha vinakidhi ipasavyo haja na mahitaji kulingana na mazingira ya wakati uliopo katika kuhabarisha umma.
Shaka amesisitiza hayo alipokuwa akizungumza na Viongozi na wafanayakazi wa vyombo hivyo katika kikao kilichofanayika leo, Jumamosi Agosti 6, 2022 katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, Jijini Dar es Salaam.
Amesema miongoni mwa hatua zilizoanza kuchukuliwa ni kuanza kwa mchakato wa kujengwa jengo ambalo ofisi za vyombo vyote vya habari vya CCM zitakuwa humo badala ya vyombo hivyo kufanyia kazi katika majengo ambayo vinalazimika kulipa kodi ya pango.
Shaka amesema lengo la ziara alizofanya katika baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, pamoja na kujenga mahausiano mema, lakini pia ililenga kujifunza na kupata uzoefu ili Chama kiweze kusimamia vyema dhamira na azma ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Samia katika kuvifanyia marekebisho na maboresho ya kimfumo vyombo vya chama ili vikidhi haja na mahitaji kulingana na mazingira ya wakati huu katika kuhabarisha umma.
“Hivi karibuni nilifanya ziara katika baadhi ya vyombo vya habari vya serikali na binafsi ili kuimarisha mahusiano yetu lakini pia kujifunza na kupata uzoefu ili tuweze kusimamia vyema dhamira na azma ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan katika kuvifanyia marekebisho na maboresho ya kimfumo vyombo vyetu vya chama ili vikidhi haja na mahitaji kulingana na mazingira ya wakati tulionao katika kuhabarisha umma” akasema Shaka.
Vyombo vya habari vya CCM ni Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Uhuru Publications Limited (UPL) Wachapishaji wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo na People's Media Communications Limited (PMCL) inayosimamia Kituo cha Radio cha Uhuru FM.
----------
Shaka akijibu hoja za wafanyakazi huku wafanyakazi wakimsikiliza kwa makini👇
No comments:
Post a Comment
ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇