LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 17, 2022

RC SERUKAMBA AWATAKA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA KUFANYA KAZI KWA WELEDI


Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba alizungumza na makarani na wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ambao wanaendelea na mafunzo katika Shule ya Sekondari ya Mwenge mjini Singida.Kulia ni  Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoa wa Singida,Naing’oya Kipuyo na kushoto ni Mratibu wa Sensa Wilaya ya Singida, Mkuki Zephania.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisisitiza jambo wakati akizungumza na makarani hao.
Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoa wa Singida,Naing’oya Kipuyo akizungumza katika mkutano huo na Mkuu wa Mkoa.
Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi wakimsikiliza mkuu wa mkoa (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.
Mkutano huo ukiendelea.
Mwakilishi wa makarani na wasimamizi hao wa Sensa Nembulisi Stephano akitoa neno la shukurani baada ya mkuu wa mkoa kuzungumza nao.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoa wa Singida,Naing’oya Kipuyo (kulia) na Mratibu wa Sensa Wilaya ya Singida, Mkuki Zephania.
Picha ya pamoja.

 Walimu ambao wapo kwenye mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa na wakufunzi wa mafunzo hayo.


Na Dotto Mwaibale, Singida

 

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amewataka makarani na wasimamizi wa sensa mkoani hapa kulifanya zoezi la kitaifa la sensa ya watu na makazi kwa uwedi na umakini wa hali ya juu.

Serukamba ameyasema hayo leo Agosti  15, 2022 wakati akizungumza na makarani na wasimamizi hao ambao wanaendelea na mafunzo katika Shule ya Sekondari ya Mwenge mjini Singida.

Alisema jukumu walilonalo nalo ni kubwa kubwa mno hivyo wanatakiwa kuhifanya kazi hiyo kwa weledi na umakini mkubwa na sivinginevyo.

“Jukumu mlilopewa ni kubwa sana mnahitajika kulifanya kwa umakini ili taifa lipate takwimu sahihi za watu kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo kuanzia ngazi ya chini” alisema Serukamba.

Serukamba aliwataka makarani hao kuzingatia yale yote wanayofundishwa badala ya kuwazia kupata posho jambo ambalo sio zuri.

"Zoezi hili la sensa la kitaifa ni kubwa na linahitaji umakini wa hali ya juu na watakalofanya lifanikiwe ni nyie hivyo msilifanye kama ni la kuja kutafuta posho,inawezekana wengine wapo hapa na vishikwambi anayofundishwa haelewi anachokifikiria ni kupata hela tu hii utakuwa hujaisaidia nchi yako," alisema.

Serukamba alisema kupitia sensa hii nchi itaweza kujua idadi ya maskini, watu wanahitaji shule,afya  na maji kiasi gani hivyo vijana watambue wameaminiwa na nchi waifanye kazi ya sensa kwa umakini sana.

Alisema mtihani kwa wasimamizi na makarani wa sensa ni kuifanya kazi kwa weledi na kuleta takwimu sahihi ambapo wakiifanya vizuri kazi hii serikali itakapokuwa na kazi nyingine wao ndo watapewa kipaumbele  kupewa.

"Mkoa unawategemea sana kupata takwimu sahihi na kuufanya uwe miongoni mwa mikoa itakayofanya vizuri katika zoezi la hili la sensa ambalo hufanyika kila baada ya miaka 10," alisema.

Serukamba alisema makarani na wasimamizi watapewa madodoso hivyo ni muhimu wajifunze mbinu za kuwauliza wananchi ili kuwafanya wawaelewe watakapokuwa wakiwadadisi.

"Kuja mtu unaweza kumuuliza una ng'ombe wangapi akashindwa kueleza pengine akidhani unataka kuja kunyang'anya ng'ombe wao ...hapana ni muhimu kujifunza mbinu za kumfanya mtu akuelewe sababu majibu yenyewe yanatokana na maswali rahisi atakayoukuzwa," alisema.

Aliongeza kwa mfano Tanzania inaelezwa ni nchi ya pili katika Afrika kwa kuwa na mifugo mingi baada ya Ethiopia lakini ukiuliza tuna ng'ombe au mbuzi wangapi hakuna anayejua.

Alisema sensa inakwenda kuleta majawabu yote hayo kinachohitajika ni umakini kwa makarani na wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi walioaminiwa na serikali kuifanya kazi hiyo.

Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoa wa Singida,Naing’oya Kipuyo alisema makarani 445 wamehitimu mafunzo yao ya dodoso la sensa ambalo watahoji majengo na makundi maalum.

Alisema kundi la pili ni la wasimamizi wa maudhui ambao watahoji dodoso la jamii ambao wapo 212 ambao wataendelea na mafunzo kwa siku tatu.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba alizungumza na makarani hao muda mfupi baada ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru 2022 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma baada ya kumaliza mbio zake mbio zake mkoani hapa  na kuridhishwa na miradi yote ya maendeleo iliyokaguliwa yenye thamani ya Sh.8.2 Bilioni.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages