MAIDA WAZIRI AAHIDI WANAWAKE WATACHAPA KAZI HAWATOMWANGUSHA
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya IBRA Contractors Limited, Maida Waziri akizungumza kwa niaba ya wakandarasi amesema kuwa wakandarasi kwa ujumla wao wanampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa serikali kuwapatia kazi nyingi za miradi ya ujenzi wa barabara nchini na kuahidi kuitekeleza kwa uzalendo.
Waziri alipata fursa hiyo ya kuzungumza wakati wa mkutano wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kutiliana saini mikataba zaidi 960 na wakandarasi wa ndani kwa ajili ya kukarabati na kujenga barabara zitakazogharimu zaidi ya sh. bilioni 300.
Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Agosti 14, 2022 ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.Aidha, Rais Samia aliiagiza TARURA na TAMISEMI, kuzingatia sheria ya asilimia 30 ya tenda za ujenzi wa barabara kuwapatia wakandarasi wanawake wenye uwezo kufanya kazi hizo kwa weredi.
Maida akiondoka baada ya kumaliza kuzungumza kwa niaba ya wakandarasi.
Maida akiwa na baadhi ya wakandarasi wanawake na wanaume.
Maida akiwa katika picha ya pamoja wakandarasi wenzake na Rais Samia na viongozi wengine.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Maida waziri akisoma risala ya wakandarasi na Rais Samia akisisitiza asilimia 30 ya kazi ya ujenzi wa barabara wapatiwe wakandarasi wanawake.....
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇