Kijana Jastine Mgaya Bina wa Kijiji cha Kaburabura, Kata ya Bugoji alichelewa kuanza masomo ya Kidato cha Tano (Form V, HGL) kwa kukosa mahitaji ya shule.
Leo, kijana huyo amepata mahitaji yote ikiwemo nauli yake ya kwenda kuanza masomo yake Nyakato High School, Bukoba.
Picha iliyoambatanishwa hapa inamuonyesha Msaidizi wa Mbunge, Vaileth Peter akiwa na kijana Jastine - wametoka Benki kufanya malipo ya shule, na tayari wamemaliza kununua vifaa vya shule, vikiwemo vitabu vinavyohitajika.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumatano, 31.8.2023
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇