LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 1, 2022

CCM KUANZA KUTOA LEO FOMU ZA WAWANIA UBUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

 Na Bashir Nkoromo,  CCM Blog

Uchuaji na urejeshaji fomu kwa Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wenye nia ya kuomba kuteuliwa na CCM kugombea Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, unaanza leo Agosti Mosi 2022 na kumalizika Agosti 10, 2022, saa 10 jioni.


Kwa wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Shaka Handu Shaka Fomu hizo zitachukuliwa na kurejeshwa  kuanzia saa 2.00 hadi saa 10:00 jioni katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Dodoma,  Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar na Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam.


Shaka alizitaja sifa za mwanachama anayestahiki kugombea nafasi hizo kupitia CCM kuwa ni;

(a) Awe ni Mwanachama hai wa CCM, (b) Awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na (c) Awe na sifa zinazostahiki kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.


(d) Awe sio Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, (e) Awe sio mtumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na (f) Awe na uzoefu uliothibitishwa au moyo wa kupenda kuimarisha na kuendeleza malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages