LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 24, 2022

ANGOLA KUKIWASHA UCHAGUZI MKUU LEO, MPLA YAPAMBANA NA UNITA, IENDELEE KUONGOZA DOLA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Baada ya Wagombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Angola kufunga kampeni zao juzi, leo Jumatano Agosti 24, Waangola zaidi ya milioni 14 waliojiandikisha kuwa wapiga kura watamchagua rais na Wabunge 220 katika Uchaguzi huo unaobashiriwa kuwa na ushindani mkali, tangu nchi hiyo iruhusu kwa mara ya kwanza Uchaguzi wa Vyama vingi mwaka 1992.

Ushindani mkali unabashiriwa  kati ya Chama cha People’s Movement for the Liberation of Angola (MPLA) chini ya Mgombea wake JoĂŁo Lourenço, ambacho kimeongoza nchi hiyo kwa nusu karne na chama cha upinzani cha National Union for the Total Independence of Angola (UNITA) chini ya mgombea wake Adalberto Costa Junior.

MPLA, kinachoongozwa na João Lourenço tangu mwaka wa 2017, kimetawala nchi ya pili kwa uzalishaji mafuta barani Afrika, tangu uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1975, hivyo kinapambana ili kuongoza tena kwa awamu ya pili.

Ushindani unaoelezewa kuweza kujitokeza ni kudaiwa kwamba chama hicho cha upinzani cha muda mrefu cha UNITA, kina nguvu zaidi kuliko hapo awali, huku yakiwepo madai kwamba wananchi wana hasira inayoongezeka kutokana na kushindwa kwa serikali kubadili utajiri mkubwa wa mafuta kuwa hali bora ya maisha kwa wote.

Utafiti wa Afrobarometer mwezi Mei 2022, ulidai idadi ya Waangola wanaopendelea UNITA, inayoongozwa na Adalberto Costa JĂşnior, imeongezeka hadi 22% kutoka 13% mwaka 2019, ikiwa ni alama saba nyuma ya MPLA. 

Rais João Lourenço, mgombea Urais kwa tiketi ya Chama tawala cha MPLA, kinachotafuta uongozi wa awamu ya pili nchini Angola.

Daladala likiwa na picha za viongozi watatu wa vyama vikuu nchini Angola na kauli mbiu "Watu wamoja, Taifa moja." Luanda, Angola, August 19, 2022

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages