LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 21, 2022

WASAFWA KUNOGESHA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO JIJINI DAR ES SALAAM.

 

 Akina mama wa Kabila la Wasafwa wakiwa katika maandalizi ya utengenezaji wa pombe ya asili ijulikanayo kwa jina la idadu itakayotumika katika tamasha la utamaduni wa kabila hilo utakaofanyika katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 hadi 24 mwezi huu. Wakwanza kushoto ni Katibu wa Wasanii wa Kabila kundi la Mbeta Rose Alufani na kulia ni Kristina Mwaniengu ambaye ametumwa na Machifu kwenda kuandaa nyumba za Asili za kabila hiyo kwaajili  ya uzinduzi utakaofanyika kesho. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

Mtaalam wa ujenzi wa nyumba za asili za kabila la wasafwa Helena Mwamengo akiendelea na ujenzi ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa tamasha la siku tatu la utamaduni wa kabila hilo utakaofanyika kesho katika kijiji cha Makumbusho kilichopo jijini Dar es Salaam. 
Wakina mama wa Kabila la Wasafwa wakiwa katika maandalizi ya utengenezaji wa pombe ya asili ijulikanayo kwa jina la idadu itakayotumika katika tamasha la utamaduni wa kabila hilo utakaofanyika katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 hadi 24 mwezi huu. Wakwanza kushoto ni Katibu wa Wasanii wa Kabila kundi la Mbeta Rose Alufani na kulia ni Kristina Mwaniengu ambaye ametumwa na Machifu kwenda kuandaa nyumba za Asili za kabila hiyo kwaajili  ya uzinduzi utakaofanyika kesho.

Sehemu ya kuishi kaya moja ya kabila la wasafwa ambayo ina   nyumba tatu tofauti yenye sehemu ya kuishi familia, kufua chuma, kihenge cha vya kuhifadhia nafaka , boma la ng’ombe na eneo la kufanyia tambiko iliyojengwa katika kijiji cha Makumbusho kilichopo jijini Dar es Salaam.

   Wasanii wa  kundi la Kabila la Wasafwa kutoka mkoani Mbeya wakiwasili katika viwanja vya kijiji cha Makumbusho kilichopo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kushiriki tamasha la utamaduni wa kabila hilo litakalofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 22 hadi 24 mwezi huu.
  Wasanii wa  kundi la Kabila la Wasafwa kutoka mkoani Mbeya wakiwasili katika viwanja vya kijiji cha Makumbusho kilichopo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kushiriki tamasha la utamaduni wa kabila hilo litakalofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 22 hadi 24 mwezi huu.
  Mhamasishaji wa tamasha  la utamaduni wa kabila la wasafwa kutoka mkoani Mbeya Reddy Makuba (Kushoto) na Katibu wa Tamasha hilo Bahati Mbwete  wakionyesha ghala la asili (kihenge) la kuhifadhia nafaka linalotumiwa na kabila hilo linalopatikana mkoani Mbeya.

  Mhamasishaji wa tamasha  la utamaduni wa kabila la wasafwa kutoka mkoani Mbeya Reddy Makuba akionyesha kamba zinazotumika kufunga mzinga wa kuhifadhia chakula unaotumiwa na  kabila  hilo linalopatikana mkoani Mbeya.
  Jiwe linalotumiwa na kabila la Wasafwa linalopatikana mkoani Mbeya kwaajili ya kusaga nafaka mbalimbali lililopo katika nyumba ya kabila hiyo katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages