LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 12, 2022

WANANCHI CHIWONDO, CHAMWINO WAPIGWA MSASA KUHUSU FAIDA ZA URASIMISHAJI ARDHI+video

 

Baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Chiwondo, wilayani Chamwino, Dodoma wakitambulishwa wakati wa mkutano wa kijiji ambao umepitisha majina ya kamati itakayokuwa inatambua mipaka wakati wa mchakato wa  kupanga mpango mji na urasimishaji ardhi ya wananchi wa eneo hilo unaoratibiwa na Mpango wa Kurasimisha Raisilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.



Viongozi wapya wa Kamati hiyo na Baraza la  Ardhi la Kijiji hicho wakipatiwa maelekezo na maafisa wa Halmashauri ya wilaya hiyo ikiwemo majukumu yao wakati wa urasimishaji ardhi na jinsi ya kutatua migogoro ya ardhi kijijini hapo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chiwondo, akifungua mkutano huo wa kijiji.

Baadhi ya wanakijiji wakishiriki katika mkutano huo ambapo walikubaliana kwa kauli moja kuanza urasimishaji wa ardhi yao.



PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, yakifanyika mafundisho hayo...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages