LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 6, 2022

SBL YADHAMINI UPANDAJI MITI 5000 HOSPITALI YA MIREMBE, DODOMA

Mbunge wa Dodoma Mjini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde akimwagilia maji mti alioupanda alipoongoza kampeni ya upandaji miti 5000 katika viunga vya Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, jijini Dodoma Julai 6, 2022.  Kampeni hiyo iliyoandaliwa na  Taasisi ya Habari Development imedhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mark Ocitti akimwagilia mti alioupanda kwenye viunga vya Hospitali ya Mirembe.
Askari Jeshi aliyeongoza vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika kampeni hiyo, akipanda mti katika eneo hilo.
Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa SBL, Katibu wa Habari Development, uongozi wa Hospitali ya Mirembe na watendaji wengine.
Naibu Waziri Mavunde (katikati) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa SBL. Kushoto ni Katibu wa Habari Development, Bernard James.
Shughuli ya upandaji miti ikiendelea.




 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Naibu Waziri Mavunde na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Ocitti wakielezea kuhusu kampeni hiyo....

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages