LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 22, 2022

RAIS SAMIA: SERIKALI YA TANZANIA IMEJIPANGA KUIMRISHA SEKTA YA BANDARI NA ANGA ILI KUKUZA BISHARA AFRIKA

Ikulu, Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imepanga kuimarisha sekta ya bandari na sekta ya anga ili kukuza biashara ndani ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Rais Samia amesema hayo leo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass) yenye urefu wa kilomita 42.4. ambayo imegharimu shilingi Bilioni 197. 4.

Aidha, Rais Samia amesema barabara hii ni muhimu kwa nchi yetu kwa kuwa ni sehemu ya barabara kuu inayounganisha kanda ya Kaskazini (Northern Corridor) hadi Holili Taveta mpakani mwa Tanzania na Kenya kuelekea Voi nchini Kenya.

Barabara hii pia inaunganisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga na Kanda mbalimbali zinazounganisha Tanzania na nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia Sudani Kusini na Sudani hadi Ethiopia.

Vile vile Rais Samia amesema kukamilika kwa barabara hii kumeimarisha sekta ya utalii pamoja na ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii katika mikoa inayopita, nchi kwa ujumla, pamoja na nchi jirani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye na viongozi wengine wakishiriki kufnya ishara ya kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022. (Picha na Ikulu).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages