LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 25, 2022

RAIS SAMIA AONGOZA SIKU YA MASHUJAA, AAGIZA LITAFUTWE ENEO KUBWA DODOMA UJENGWE MNARA MKUBWA WA MASHUJAA+video

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka silaha za jadi (Ngao na Mkuki) kwenye mnara wa Mashujaa kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jacob Mkunda akiweka sime kwanye mnara wa  mashujaa
Kiongozi wa mabalozi wa Nchi za Nje nchini, akiweka shada la maua.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Davis Mwamfupe  akiweka upinde na mshale kwenye Mnara wa Mashujaa.
Muwakilishi wa Tanzania Legion, Mzee Omari Mhando Shangali (102) ambaye alipigana vita ya Pili ya Dunia akipiga Salute kutoa Heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuweka Shoka kwenye mnara wa Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (katikati) akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Fatma Maganga (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalumu,  pamoja na viongozi wengine wakati wa maadhimisho hayo.
Baadhi ya viongozi wa CCM wakishiriki maadhimisho hayo.
Sehemu ya wananchi walioshiriki maadhimisho hayo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti yaUtumishi wa Umm, Deo Ndejembi (katikati) akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaude Kighahe. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mbarouk Nassor.


PICHA ZAOTE NA RICHARD MWAIKENDA








No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages