LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 28, 2022

RAIS SAMIA ACHEKECHA WAKUU WA MIKOA, ATEUA WAPYA 9, KUHAMISHA 7 NA KUWABAKIZA 10 AKIWEMO AMOS MAKALLA

Ikulu, Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa Wapya tisa (9) na kuwahamisha vituo vya kazi Wakuu wa Mikoa saba (7) huku wengine kumi (10) akiwabakiza kwenye vituo vyao.

Taarifa iliyotolewa leo Julai 28, 2022 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Dodoma, imesema,  Wakuu wapya wa mikoa na mikoa wanayoshika ikiwa katika mabano ni, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha Nurdin Hassan Babu (Kilimanjaro) na Fatma Abubakar Mwasa (Morogoro).

Halima Omari Dendego (Iringa), Dk. Raphael Masunga Chegeni (Mara), Peter Joseph Serukamba (Singida), aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani Kanali Ahmed Abbas Ahmed (Mtwara) na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Kanali Laban Elias Thomas (Ruvuma).

Taarifa hiyo ya Ikulu imewataja waliohamishwa vituo vya kazi na mikoa yao mipya ikiwa kwenye mabano kuwa ni; aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony John Mtaka (Njombe), aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Cuthbert Sendiga (Rukwa) na  aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Waziri Kindamba (Songwe).

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Martin Reuben Shigella (Geita), aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Songwe    Omary Tebweta Mgumba (Tanga), aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Tanga Adam Kigoma Malima (Mwanza) na aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemary Staki Senyamule (Dodoma).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanaoendelea kuwa kwenye Vituo vyao vya kazi na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni; Amos Gabriel Makalla (Dar es Salaam), John Vianney Mongella (Arusha), Mwanamvua Hoza Mrindoko (Katavi), Charles Makongoro Nyerere (Manyara) na Zainab Rajab Telack (Lindi).

Juma Zuberi Homera (Mbeya), Thobias Emir Andengenye (Kigoma), Sophia Edward Mjema (Shinyanga),    Balozi Batilda Salha Burian (Tabora) na Abubakar Mussa Kunenge (Pwani).

"Uapisho utafanyika Ikulu Chamwino, Dodoma tarehe 1, Agosti, 2022", Amesema Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus, katika taarifa hiyo.

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kazini

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages