Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameagiza mamlaka za serikali za mtaa kuendelea kuwezesha vijana kupata mikopo pamoja na uwezeshaji wa miundombinu kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Prof.Ndalichako amebainisha hao leo Julai 27,2022 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ufungaji wa program ya Feed the Future Tanzania inua vijana chini ya ufadhili wa shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa[ USAID].
Aidha,Prof.Ndalichako amesema Programu ya The Future imetumia zaidi ya Tsh.Bilioni 8 katika kuwezesha vijana na kuhimiza USAID kupanua wigo kwa mikoa mingine ili kuwezesha vijana wengi kushiriki kuleta maendeleo hapa nchini.
Katika hatua hatua nyingine Prof.Ndalichako amesema serikali imeanza mchakato wa ujenzi wa vituo vitano kwa ajili ya kuendeleza vijana.
Mkurugenzi wa utawala kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Victor Kategure amesema Mradi wa Programu ya Feeda the Future Tanzania inua vijana umetekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano tangu mwaka 2017 hadi sasa ukilenga vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35.
Mkurugenzi mkuu shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa [ USAID] nchini Tanzania,Kate Somvongsiri takriban vijana laki nane [800,000 wanaingia katika nguvu kazi ya Tanzania wakiwa na matarajio madogo sana au hata bila matarajio ya kupata ajira.
Aidha ,amesema serikali ya Marekani imekuwa ikishirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha vijana wainua uchumi wao ambapo amesema ni muhimu vijana kupewa ujuzi na ushirikishwaji kwenye sekta ya kilimo ambapo karibu asilimia 67 ya nguvu kazi ya Tanzania inajishughulisha na kilimo.
Ufungaji wa Programu ya Feed the Future Tanzania Inua Vijana umekwenda sambamba na kaulimbiu isemayo “Vijana ni Nguvu Kazi ya Taifa”ambao ulikuwa umejikita zaidi katika mikoa ya Mbeya ,Iringa , na visiwani Zanzibar katika kuwainua vijana kiuchumi kupitia miradi ya kilimo na ufugaji ambapo zaidi ya vijana 43,000 wamepata mafunzo ya ujasiriamali,utayari na nguvu kazi ,uongozi na stadi za maisha kwa ajili ya kuishi na kupanga maisha bora.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇