LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 25, 2022

LEO NI LEO CCM WAZAZI PANGANI





























Na Dismas Lyassa, Kibaha 

WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) 25 wamepitishwa na vikao mbalimbali vya CCM kugombea nafasi mbalimbali katika Kata ya Pangani, Kibaha Mjini Mkoani Pwani. 


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na kusainiwa na Siffer Sharon Tulliy (pichani kulia), Katibu wa Wazazi Wilaya Kibaha Mjini, jumla ya wagombea watatu wamejitokeza kugombea Uenyekiti wa Jumuiya hiyo ambao ni Kassim Hamza Nguku, Yusuf Khalfan Elecrosh na Amir Msangi.


 Aidha katika nafasi ya Ukatibu, wagombea ni Jackson Peter Msaki, Khadija Thabiti Mbala na Augustino Nchimbi, huku wagombea wa nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu kata CCM kutokea wazazi wakitajwa kuwa ni Protas Charles Mtei, Asimwe Mendane na Tua Ramadhani Kassim.

 

Wagombea wa nafasi ya Elimu, Malezi na Mazingira ni Zainabu Amrani Kaduma, Steven Emera na Asha Kilimila. Aidha nafasi ya baraza wagombea ni Hamad Mdohole, Mwanahamisi Mangu, Khalid Mohammed Bwellah, Viktoria Mwankenja, Rehema Selemani na Mohammed Mrema.


 Nafasi imegombewa na wana CCM watatu, huku nafasi ya uwakilishi wa UWT ikigombea na wawili ambao ni Mwanahamisi Mangu na Halima Ramadhan. Sophia Haji Stambuli na Mwanahamisi Chitundu wamegombea uwakilishi UVCCM.


 Wanachama na wagombea wote wameaswa kuzingatia kanuni na katiba ya chama katika kuhakikisha amani na utulivu unatawala.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages