LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 25, 2022

KINANA: VIJANA NA WANAWAKE GOMBEENI UCHAGUZI NDANI YA CCM, HAKUNA SULTANI WA KUONGOZA MILELE

Mpanda, Katavi
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amewataka wanawake na vijana nchini kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania nafasi za ungozi ndani ya Chama na kuwahakikishia kuwa haki itatendeka.

Amesisitiza kuwa Wanawake na Vijana hao wajitokeze bila hofu yoyote kwa sababu ni haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa na kwamba hawana sababu ya kuwa na hofu akisema hakuna wa kumtisha mwenzake.

Kinana ameyasema hayo mjini Mpanda mkoani Katavi, wakati akizindua mradi wa fremu 15 za maduka zilizojengwa katika Ofisi za CCM za mkoani humo, ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia uchaguzi unaoendelea ndani ya CCM.

Akifafanua zaidi Kinana amesema, uchaguzi ndani ya Chama upo katika hatua mbalimbali hivyo mbali na Wanawake na Vijana ni vyema wana CCM wakajitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili kuwania nafasi za uongozi.

Kinana amewapa moyo Wanawake akisema, "Niwaombe kina mkachukue fomu msiogope, nendeni mkachue fomu mpambane na wanaume.

"Nataka niwasihi vijana gombeeni hizo nafasi, uchaguzi ukija nafasi zitakuwa wazi na kila mtu atakuwa na haki sawa na mwenzake, hakuna masultani wa kukaa madarakani milele, tuna uchaguzi kila baada ya miaka mitano, wenye kuwachagua viongozi ni wana CCM, wakikupenda, wakikuheshimu na wakithamini mchango wako watakupa kura, wasipothamini watakunyima kura.

"Nafikiri na ninyi mnawafahamu wajumbe sio watu wazuri, wanaweza kukwambia usiwe na wasiwasi tutakupa kura, halafu baadae unatoka kapa, hivyo niwaombe sana vijana gombeeni, kina mama gombeeni, tutatenda haki, hatutampendelea mtu, wala mtu asimtishe mwenzake, kwamba ukienda kuchukua fomu unaambiwa na wewe unatafuta nini, kwani na wewe ulivyochukua fomu mwingine sialikuwepo kabla yako, ndio umechukua nafasi yake na mimi nakuja kukung'oa wewe," alisema.

Kanali Mstaafu Kinana alisema Chama kitazingatia demokrasia na hakitampendelea yeyote katika uchaguzi huo ili kuwapata viongozi wenye kukubalika.
===

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa fremu 15 za maduka zilizojengwa katika Ofisi za CCM ya CCM mkoa wa Katavi, akiwa katika ziara ya Kikazi mkoani humo, leo. Picha zaidi za hekaheka ya ziara hiyo👇👇




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages