LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 30, 2022

KIBOKO DUME ALIYEKUWA AKISUMBUA WANANCHI SAME AUAWA KWA KUPIGWA RISASI




 Kiboko dume ambaye kwa muda mrefu amekuwa akisumbua Wananchi wa Kata ya Mabilioni Wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro na kukwamisha shughuli za maendeleo kama  kilimo, ufugaji na uchotaji wa maji katika Mto Pangani ameuawa kwa kupigwa risasi katika msako ulioongozwa na vikosi kutoka TAWA 


Kiboko huyo aliyepewa jina la Babu ambaye ameua jumla ya Watu  6, zaidi ya ng’ombe 8, punda na mbuzi tangu mwaka 2017  alikuwa akihusishwa na imani za kishirikina kwani jitihada mbalimbali za kumdhibiti hazikufanikiwa katika kipindi chote


Tarehe 17 Juni 2022 kiboko huyo alimuua kwa kumshambulia Mwanaume mmoja aliyekuwa anakwenda shambani kumwagilia ndipo Mkuu wa Wilaya ya Same, Edward Mpogolo alipoagiza kuhakikisha kila mbinu zinatumika kumuua Kiboko huyo ili Wananchi warudi kufanya shughuli za maendeleo kwa amani


Baada ya kuanza msako kiboko huyo aliuawa tarehe 28 Julai 2022 saa 11 alfajiri baada ya kuweka mtego na kupigwa risasi ya kichwa na Mzee Ally Miraji Sengela (Hunter) aliyesaidiwa na Mzee Fue Omary Ngerwa (Mvuvi na Mweka Mtego) kwa kushirikiana na wahifadhi wa TAWA.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages