LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 9, 2022

HOSPITALI YA ROYAL POLYCLINIC YAZINDULIWA DAR, MEYA KUMBILAMBOTO AWAPONGEZA KWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

Na Bashir Nkoromo, Blog ya Taifa ya CCM
Viongozi wa Hospitali ya Royal Polyclinic iliyoanzia Zanziabr wamepongezwa kwa kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan za kuimarisha huduma za Afya Nchini.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto, ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa Hospitali ya kisasa ya Royal Plyclinic kwenye jengo lililopo eneo la Mnazi Mmoja jijini.

"Kwa kweli nawapongeza sana ninyi viongozi wa Hospitali hii ya Royal Polyclinic kwa uamuzi wenu wa kuweka hospitali hii Tanzania Bara, tena hapa katikati ya Jiji hili la Dar es Salaam.

Jambo hili mumefanya jema sana, maana hatua hii mmemuunga mkono Rais wetu Samia Suluhu Hassan katika jitihada zake ambazo amekuwa akizifanya katika kuhakikisha huduma za wananchi wake zinakuwa bora kila kona ya nchi yetu", akasema Kumbilamoto.

Amesema kupatikana kwa hospitali hiyo katika eneo la Mnazi Mmoja kutasaidia Hopsitali ya Serikali ya Mnazi Mmoja kupumua japo kidogo kwa kuwa ndiyo pekee kubwa iliyokuwa inatoa huduma katika eneo hilo.

Kumbilamoto amesema, pamoja na kusaidia huduma za matibabu, lakini pia hospitali hiyo imekuwa msaada kwa kutoa ajira kwa zaidi ya wafanyakazi 40.

Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Ahmed Suleiman alisema, kabla ya kuwa Hopsitali Royal Polyclinic ilianzishwa Zanzibar eneo la Kiembesamaki ikiwa ni Duka la Dawa tu.

 "Mwanzo  tulianza na 'Pharmacy' ambayo ipo Kiembe Samaki Zanzibar mwaka 2004, baadaye tukaona  uhitaji wa huduma zetu kwa wananchi umekuwa mkubwa, tukaamua ndipo tukaja na wazo la kutanua huduma zetu na kuwa na 'Clinic' inayotoa huduma za kibngwa katika fani mbali mbali za kitabibu na huduma za meno.

Tulianza wawili tukaja hadi saba tunatoa huduma za dawa na vipodozi na ushauri. Tulikuwa tunafunga saa nne usiku, ikaja saa sita usiku sasa tunatoa huduma kwa saa 24", akasema Mkurugenzi huyo na kuongeza;

"Mwaka 2019 tulianza rasmi hopsitali ya Royal Medical Clinic ambayo pia ni Polyclinic. Tulianza na Wafanyakazi  20 na kufikia 40 tulio nao sasa, lakini wengi wao ni 'part time'.

Tuna 'Paharmacy, Maabara ya kisasa, tunatoa na huduma ya meno, madaktari tulio nao  ni 'Gynacologist', 'Phycison', 'Pediatrition', nephrologist', na 'Heamotologist'.

Pia tunatoa huduma ya Consultation kwa wagonjwa wa vidonda vya sukari na wale wanaotaka ufafanuazi juu ya hali yao ikiwa wanataka huduma mbadala".

"Huduma ya Hospitali tulianza mpaka saa 3 usiku ikaja saa 6 usiku na sasa ni saa 24. Hatulazi wagonjwa, tunatoa huduma za Bima za Afya za NHIF na pia tumeanza kuzungumza na  Jubilee.

Kwa sasa tunahudumia zaidi ya wagonjwa 2,800 hadi 3,000 kwa mwezi, kwa mwaka ni wagonjwa 33,600 hadi 36,000 kwa wakati mwingine hadi wagonjwa 40,000 na wanaotumia Bima ya Afya 1,400 hadi 1,700 kwa mwezi.

Sisi tunatoa huduma kwa kila mtu, tumekuwa na uhaba wa eneo, tulijaribu tulipate lakini ikashindikana kutokana na hali, tunatarajia kupata eneo ili kupanua huduma".

Kuhusu changamoto Mkurugenzi huyo alisema, wanakabiliwa na jengo waliweka Hospitali yao wamepanga na kuna changamoto kadhaa ikiwemo uhaba wa maegeso ya magari na ufunyu wa eneo.

"Tunaomba Halmashauri ya Jiji itupe au itufikirie kutupa eneo ambalo tunaweza kujenga Kituo kikubwa zaidi cha Afya na kwa hapa tulipo tupewe eneo la maenegesho kwa ajili ya wagonjwa", alisema Mkurugenzi huyo kwa Meya Kumbilamoto.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto akizindua Hospitali ya  Royal Polyclinic eneo la Mnazi Mmoja Jijini, leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Ahmed Suleiman.


Habaripicha: Mwanzo hadi mwisho wa shughuli👇

Mkurugenzi wa Hospitali ya Royal Polyclinic Ahmed Suleiman akisalimiana na Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto wakati akimpokea Meya huyo alipowasili kufungua hopsitali hiyo, leo. Kulia ni baadhi ya Viongozi wa hospitali hiyo.
Meya Kumbilamoto akizungumza kidogo na Viongozi wa Hospitali hiyo.
Meya Kumbilamoto akipiga shoto kulia kwenda eneo la tukio huku akisindikizwa na Viongozi wa Hospitali hiyo.
Meya Kumbilamoto akiwa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Royal Polyclinic Ahmed Suleiman.
Meya Kumbilamoto akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ofisini kwa Mkurugenzi wa hospitali hiyo (aliyesimama)
Meya Kumbilamoto akiwa amepumzika na viongozi wa Hospitali hiyo kabla ya kuanza shughuli ya uzinduzi.
Meya Kumbilamoto na Mkurugenzi Ahmed wakifurahia maongezi ya hapa na pale wakati wamepumzika kabla ya shughuli ya uzinduzi
'Ratiba yetu ndiyo hii", Mmoja wa Waratibu shughuli ya uzinduzi wa Hospitali hiyo akimwambia Meya Kumbilamoto.
" Ohh, Mzee shikamoo", akasema Meya Kumbilamoto wakati akisalimiana na Mzee Suleiman Mohammed Rashid.  Kisha Kumbilamoto akapita kwenye maonyesho ya bidhaa za dawa mbalimbali zinazopatikana kwenye Pharmacy za Hospitali ya Royal Polyclinic👇
👇
👇
👇
Mmoja wa Viongozi wa Hospitali hiyo akifanya Utambulisho
Meya Kumbilamoto akiteta jambo na Mkurungzi Ahmed.
Meya Kumbilamoto akiendele kuteta jambo na Mkurungzi Ahmed.
Afisa Mawasiliano wa Hospitali hiyo Nawha Ahmed akisoma risala.
Kisha Nawha akakabidhi risala hiyo kwa Meya Kumbilamoto
Mkurugenzi Ahmed akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi kuhutubia na kuzindua Hospitali hiyo.
Meya Kumbilamoto akizungumza.
Mmoja wa Viongozi wa Hospitali hiyo Mohamed Seif Nasoro akizungumza kutoa neno la Shukurani kwa mgeni rasmi Meya Kumbolamoto
Kisha Meya Kumbilamoto akaenda eneo la tukio na kukata utepe kuashirikia kuizindua Hospitali hiyo. Kisha akapelekwa kuona baadhi ya maeneo ya utoaji huduma katika Hospitali hiyo👇
Eneo la huduma ya Pharmacy
Eneo la Huduma ya meno.
Eneo la mapumziko ya Wagonjwa.
Eneo la Maabara.
Meya Kumbilamoto akizungumza na Mkurugenzi Ahmed wakati wakisubiri chakula cha mchana kwenye hafla hiyo.
WAFANYAKAZI NA WAALIKWA MBALIMBALI WAKIWA KWENYE HAFLA HIYO👇
UKAWADIA MUDA WA 'KUJISEVIA' CHAKULA AKIONGOZA MEYA KUMBILAMOTO👇
Baada ya chakula cha mchana ndiyo ukawa mwisho wa hafla hiyo.                                               ©July 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo 
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages