LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 8, 2022

DIWANI WA CCM KATA YA MAJOHE WLAYANI ILALA AFARIKI DUNIA AKIWA MSIKITINI, LEO ALFAJIRI

Na Heri Shabani, Ilala

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, kimepata pigo kufuatia Diwani wake wa Kata ya Majohe Mohamed Ngonde, kufariki leo alfajili akiwa msikitini.

Akizungumza kwa njia ya simu Katibu wa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Busoro Pazi, alisema Marehemu Mohamed Ngonde alifariki akiwa Msikitini katika Ibada ya alfajili Leo Julai 08/2022.

Katibu wa Madiwani Busoro Pazi alisema taratibu za mazishi bado kila wakati atakuwa anatoa taarifa baada kukaa na familia ya marehemu.

"Kwa Sasa tunafanya taratibu za kwenda kuifadhi mwili wa marehemu katika hospitali ya Rufaa Mkoa Amana "alisema Busoro.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde alisema taarifa za Kifo cha MH, Diwani wake Mohamed Ngonde aliyefariki alfajili katika alizipata kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM kata Majohe ambapo alisema alimweleza kuwa Marehemu Mohamed Ngonde alifariki ghafla.

Mwenezi CCM Wilaya ya Ilala Alhaj Said Sidde alisema kila wakati atakuwa anatoa taarifa kamili kuhusiana na msiba huo mzito kwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na wana CCM kwa ujumla.

Alhaj Said Sidde,pia ongeza kuwa alimwelezea Ngonde kuwa kada mahiri aliyekitumikia Chama Cha Mapinduzi kwa muda mrefu na kushikilia nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti serikali ya mtaa Kichangani, Majohe

Mohamed Ngonde

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages