LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 5, 2022

WANANCHI KISILO KUANZA KUPATA UMEME JULAI

Na Mwandishi wetu,Njombe


Baadhi ya vijiji vya kata za Lugenge na Iwungilo wilayani Njombe ambavyo havina nishati ya umeme vimeripotiwa kwenda kupata nishati hiyo katika siku za usoni baada ya kukosa nishati kwa miaka mingi.

Kupitia ziara ya kikazi ya mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa katika kata mbalimbali, wakala wa umeme vijijini REA chini ya msimamizi wa miradi hiyo mkoa wa Njombe Mhandisi Nicholas Lazaro amesema kwenye baadhi ya vijiji vitaanza kupelekewa nishati hiyo ndani ya siku nne na vingine mwezi mmoja.

"Tumeshafanya upembuzi baada ya diwani kutuletea vijiji hivi na michoro ipo REA kwa hiyo kwa haraka haraka baada ya mwezi mmoja naamini bapa tutaanza"amesema Mhandisi Nicholas Lazaro

Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema atahakikisha anaendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo ya umeme mpaka wananchi wapate nishati hiyo.

"Kwa hiyo tarehe tatu mwezi wa Saba mimi na mhandisi tutakuja tena hapa kwasababu tumesibiri Sana"alisema Kissa Kasongwa

Baadhi ya wakazi wa Kisilo kata ya Lugenge na Iwungilo akiwemo Leo Mwinuka na Isdory Mligo Wamesema Kukosekana kwa umeme kuendelea kuwakwamisha pakubwa na kuwaingizia hasara kubwa.

FIloteus Mligo ni Diwani wa kata ya Lugenge ambaye anasema atakuwa bega kwa bega kuhakikisha hujuma hazifanyiki katika miradi hiyo kama ilivyowahikufanyika kipindi kilichopita kwani zilipelekwa nguzo za umeme na Kisha kuondolewa Tena.

Ziara ya mkuu wa wilaya ya Njombe inaendelea katika kata mbalimbali kwa kufanya mikutano ya hadhara,kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages