Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara ameahidi kuendelea kutetea bungeni maboresho ya maslahi ya wabunge hadi kieleweke. Ametoa ahadi hiyo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezi madiwani wote kutoka Tarime Vijijini yaliyofanyika Royal Village jijini Dodoma Juni 17, 2022. Aidha ameiomba serikali kuweka utaratibu wa kuwaandalia mafunzo ya kuwajengea uwezo madiwani ili waweze kusimamia vizuri miradi mbalimbali katika Kata zao.
Waitara akipongezana na Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Mara, Gati Chomete baada ya mafunzo ya madiwani kufungwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime Vijijini, akitoa shukrani kwa Mbunge Waitara kwa kufanikisha mafunzo hayo.
Madiwani wakisikiliza kwa makini wakati Waitara akizungumza nao.Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Waitara akitoa ushauri wake huo...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇