Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, jana walinogesha Kikao chao cha mwisho cha Baraza hilo kwa kumshirikisha mmoja wa Waasisi wakongwe wa Jumuiya hiyo Mama Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa kwanza Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
Ili Mama Maria aweze kushiriki kama mwalikwa kwenye kikao hicho, timu yote ya Wajumbe wa Baraza hilo wakiongozwa na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga, walifunga safari hadi nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, Msasani Jijini Dar es Salaam.
Katika msafara huo, Mwenyekiti Masunga aliambatana na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Paulina Bupamba, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Madiwani wa Viti Maalum kupitia UWT na Wajumbe wa Baraza la Utekelezaji UWT na Mwenyekiti na Makatibu wa UWT wa wilaya zote tano za mkoa huo.
"Mama , Mama Maria Nyerere, wewe ndiye muasisi wa sisi wanawake wanawake kutambulika kikanuni na kiutaratibu kama alivyosema Katibu wetu wa UWT mkoa, ni kiutaratibu huwa tunawaalika Waasisi kwenye Baraza letu la mkoa, lakini kutokana na hali halisi ya Bibi tumeona kwamba yeye asitufuate, sisi Wajumbe wa Baraza ndiyo tumfuate kama tulivyofanya.
Kwanza tumefurahi, tumecheka, tumefurahi kwa pamoja, lakini pia umetupa nasaha nzuri kwa hiyo kimsingi pamoja na kuja kukushirikisha kwenye kikao hiki tumekuja kuchota busara zako", akasema Mwenyekiti Masunga wakati akitoa shukrani baada ya Mama Maria kuzungumza.
Akizungumza kwa taratibu kutokana na umri wake, Mama Maria Nyerere mwenye umri wa amiaka 92, aligusia mshikamano, upendeo na kufanya kazi za uzalishaji.
Licha ya kuzungumza taratibu katika mazungumzo hayo, Mama Maria Nyerere aliweza kukonga nyoyo za Wajumbe hao wa UWT kwa kuwaeleza kwa utani mikasa midogo midogo ya kimaisha lakini yenye ujumbe mzito, na kuwafanya Wajumbe hao wakati fulani kuagua kicheko sanjari na yeye.
Baadaye Wajumbe hao waliondoka na kwenda katika Ukumbi wa Arnautouglo kuendelea na kikao hicho cha Baraza ambapo walijadili agenda mbalimbali na kisha kutoka na maazimio.
Mwenyekiti Mmasunga, Katibu Bupamba na M-Mnec Akilmali waliwaasa wajumbe kwamba pamoja na kwamba kikao hicho ni cha mwisho kutokana na uchaguzi ndani ya chama kuwadia, lakini bado ni viongozi hivyo waendelee kumsaidia Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan kwa kueleza yale mema ya maendeleo ya Taifa anayoyafanya.
Mama Maria Nyerere akizungumza wakati wa Kikao cha Baraza la UWT mkoa wa Dar es Salaam kilipoanzia nyumbani kwake Msasani, jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT mkoa huo Florence Masunga na Kushoto ni Mjumbe wa NEC ya CCM Angelina Akilimali na Katibu wa UWTMkoa huo Paulina Bupamba. Mama Maria Nyerere akiwa na badhi ya viongozi na Wajumbe wa Baraza la UWT mkoa wa Dar es Salaam, nyumbani kwake Msasani.
Mama Maria Nyerere akiwa na badhi ya viongozi na Wajumbe wa Baraza la UWT mkoa wa Dar es Salaam, nyumbani kwake Msasani. Picha zaidi baadaye
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇