LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 3, 2022

UWT DAR WAGAWA TAULO ZAIDI YA 750 ZA KIKE KWA WANAFUNZI SARANGA, WALAANI MATUKIO YA WANAUME KUUA WAKE ZAO NA MSICHANA WA NDANI KUNYONGA MTOTO

Na CCM Blog, Saranga, Ubungo
Viongozi wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, wamegawa taulo zaidi ya 750 za kike kwa Wasichana wa Shule ya Sekondari ya Saranga Wilayani Ubungo, huku wakilaani tukio la kunyongwa mtoto na msichana wa kazi na vitendo vya wanaume kuua wake zao vilivyokithiri.

Pia viongozi pamoja na kuwapatia taulo za kike wamewafunda wanafunzi wa kike wa shule hiyo ya Saranga kujikita katika masomo na kujiepusha mambo ya hovyo ambayo yatawasababisha kushindwa kutimiza ndoto zao za kufanikiwa kimasomo na kuja kuwa miongoni watakaolisaidia Taifa kufanikiwa katika nyanja mbalimbali.

Viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga, Katibu wa UWT wa mkoa huo Paulina Bupamba na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, wamegawa taulo hizo za kike na kuyasema hayo katika hafla iliyofanyika katika shule ys Sekondari ya Saranga, jana.

"Bila shaka wanangu mnamjua Rais wetu Mheshimiwa Suluhu Hassan", Mwenyekiti Florence akawauliza Wasichana wa Shule ya Sekondari ya Saranga nao wakajibu, "Ndiyoooo". Akasema;

"Kama mnavyomjua kuwa ni Mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Nchi yetu na ameonesha utendaji kazi uliotukuka, sasa ninyi hamna ndoto ya kuwa Samia?" Wanafunzi wote wa kike ambao ndiyo pekee walioitwa kweneye hafla hiyo wakanyoonya mikono juu na kusema "tunayoooo".

"Basi kama mna ndoto za kuwa Samia na kuwa viongozi mbalimbali watakaolijenga Taifa letu la Tanzania  hakikisheni mnazingatia masomo kwa bidii na kuachana kabisa na mambo ya hovyo yatakayozuia kutumiza ndoto zenu", akasema Mwenyekiti Florence Masunga.

"Pia naomba kutumia nafasi hii, kutamka kwamba, UWT mkoa wa Dar es Salaam, tunalaani na kukemea vikali tukio lililotokea katika Kata hii ya Saranga la Msichana mfanyakazi wa ndani kumuua mtoto asiye na hatia kwa kumnyonga.

Pia tunalaani na kukemea vikali matukio ya wanaume kuwaua wake au wenza wao kwa njia mbalimbali ikiwemo kutumia risasi ambao yanaonekana kushamiri, tunaiomba Serikali ichukue hatua za kisheria dhidhi ya wanaohusika na matukio haya ambayo yanalidhalilisha taifa letu", akasema Mwenyekiti Florence Masunga na kuongeza;

Wakati tunalaani hii kadhia ya Wanaume kuwaua wake zao, tunawaasa pia wanawake kuwaheshimu waume zao, kama vitabu vinavyosema, na wanaume wawaheshimu wake zao pia kama vitabu vinavyosema, maana tunaamini hili likizingatiwa katika jamii zetu mauaji haya yatapungua au kuisha kabisa.

Kwa upande wake Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Paulina Bupamba akiwafunda wanafunzi hao wa kike, aliwataka kukwepa kabisa kujihusisha na mambo ya mitandao ya Kijamii na badala yake kuzingatia masomo ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao.

"Mnajua watoto, hii mitandao ya kijamii inaharibu sana ufuatiliaji wa masomo, kwa hiyo hakikisheni kila mmoja wenu anaikwepa na kuzingatia masomo yake, maana ukizingatia masomo, kisha ukafaulu vizuri ndiyo njia pekee ya uhakika itakayokuwezesha wewe mtoto wa kike kutimiza ndoto zako", akasema Katibu Paulina Bupamba, huku wanafunzi hao wakimshangilia kuonyesha kuyakubali maneno yake.

Naye Mjumbe wa NEC Angelina (Angel) Akilimali pia aliwaasa wanafunzi hao kuwepa vishawishi ambayo huwakumba wanafunzi wa kike ikiwemo vijizawadi vya vyakula ikiwemo chipsi, usafiri wa bure wa bodaboda na kujihusisha na makundi ya wale wasichana na wavulana wa mitaani wasiojua umuhimu wa masomo.

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Angelina (Angel) Akilimali wakigawa taulo za kike kwa Wanafunzi wa shule ya Sendari Saranga, Wilayani Ubungo Jijini Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Katibu wa UWT mkoa huo Paulina Bupamba. katika tukio hilo UWT waligawa taulo hizo kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 70.  

Mwanzo👇

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, akiwa amepumzika na viongozi wenzake baada ya kufika katika Shule ya Sekondari ya Saranga tayari kwa shughuli hiyo ya kugawa taulo za kike na kuzungumza ana wanafunzi wa kike wa shule hiyo. Baadhi ya wengine ni Kushoto ni Mjumbe wa NEC Angelina (Angel) Akilimali na Katibu wa UWT mkoa huo Paulina Bupamba.
Viongozi wa UWT mkoa wa Dar es Salaam wakizungumza jambo na Katibu wa UWT Wilaya ya Ubungo Mazoea Salum kabla ya hafla kuanza.
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Paulina Bupamba akizungumza kufanya utambulisho na kuwaalika viongozi kuzungumza na wanafunzi katika shule hiyo ya sekondari Saranga
Mjumbe wa NEC Angelina (Angel) Akilimali akizungumza na wanafunzi wa kike wa shule hiyo ya Saranga.

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, akizungumza na wanafunzi wa kike wa shule hiyo ya Saranga.
Wanafunzi wa kike wa shule hiyo ya Saranga wakimshangilia Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga wakati akizungumza nao.
"Watoto, UWT tupo nanyi, hatuwatupi?" Katibu Paulina Bupamba akiwaambia wananfunzi hao.
Wanafunzi waghani shairi kutumbuiza ugeni wa Viongozi wa UWT mkoa wa Dar es Salaam katika hafla hiyo.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Saranga Nsembo Kuandika akitoa neno la shukrani kwa Viongozi wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, mwisho mwa hafla hiyo.
Mwanafunzi Vivian Valentino Manji akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake wa kike kwa Viongozi wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, mwisho mwa hafla hiyo.
Katibu wa UWT Wilaya ya Ubungo Mazoea akitoa neno la shukrani kwa Viongozi wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, mwisho mwa hafla hiyo.
"Nadhani shughuli yetu imefana, au unaonaje?" Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Paulina Bupamba akamuuliza Mkuu wa Shule ya Saranga Nsembo Kuandika wakati wakiagana baada ya shughuli hiyo.
"Hakikisheni jamani mnawasaidia vya kutosha watoto hawa kusoma vizuri masomo yao", kasema Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga wakati akiagana na Mkuu wa Shule hiyo Mrs Kuandika.
"Byee", wanafunzi wa shue ya Saranga wakimsindikiza Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Paulina Bupamba wakati akiondoka baada ya shughuli kumalizika.

"Haya Mwalimu, sisi tunaondoka, tutarudi siku nyingine tunawatakia kila la heri katika mapambano haya ya kuwafkisha watoto wetu katika ndoto zao", akasema M-NEC Akilimali wakati akiagana na Mkuu wa Shule ya Saranga baada ya hafla hiyo.

© June 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages