Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amegawa baadhi ya vifaa vitakavyowezesha usajili wa wanachama Kidigital jimboni hapo.
Ridhiwani ametoa vifaa hivyo katika kata 15 ambazo zote zipo jimbo la Chalinze Mkoani Pwani, wakati aliposhiriki vikao vya CCM wilaya.
Alisema mtaji wa chama chochote ni wanachama ,hivyo ongezeko la wanachama Tena kusajiliwa kidigital ni muenendo muzuri katika kujiimarisha Chama.
Ridhiwani alisisitiza Chama ni umoja na mshikamano ,kwani CCM itajengwa na wanachama wenyewe.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇