LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 20, 2022

M-NEC KINONDONI: MNAOSHINDA NA MNAOSHINDWA HAKIKISHENI MNAENDELEZA MSHIKAMANO KUKIJENGA CHAMA SIYO KUSUSA NA KUNUNIANA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni Mussa Omari amesema wanaoshinda na wanaoshindwa katika uchaguzi wanapaswa kuhakikisha wanaendelea kuwa na Umoja na mshikamano katika ujenzi wa CCM badala ya kususa na kununiana.

M-NEC huyo ameyasema hayo jana, akiwa mgeni rasmi katika hafla ya viongozi wapya na Wanachama wa CCM tawi la Kibomu, Kata ya Kawe wilaya ya Kinondoni mjini Dar es Salaam, kupongezana kwa kukamilisha vizuri Uchaguzi wa ndani ya Chama uliofanyika hivi karibuni katika tawi hiyo.

"Kama kweli ulikuwa umeomba nafasi ya Uongozi kwa nia hasa ya kukitumikia Chama, na ikatokea kwamba uemeshindwa katika uchaguzi usisuse na kununa kwa sababu, mnyenyekee aliyekuekushinda na ujitahidi kuonyesha mshikamano na kuendelea kukitumikia chama kwa uaminifu.

Unajua unaposhindwa na ukaendelea kushikamana na wenzako ndani ya Chama na kuongeza uadilifu, siri yake ni kwamba kufanya hivyo kutakujengea sifa njema ambayo itakufanya viongozi na wanachama wenzako wakuone kuwa ni mvumilivu na hivyo kupita wakati wa uchaguzi mwingine.

Unapohitaji kuwa kiongozi unatakiwa kuwa mvumilivu, siyo ukikosa mara moja au hata mara nyingi unatokwa na maneno makali, kejeli na kususa, hiyo haifai, hivi mnavyoniona nikiwa Mjumbe wa NEC, nimepita vikwazo vingi kila nilipokuwa nagombea nafasi mbalimbali, lakini nikatulia, sasa ningejifanya jeuri leo msingeniona hapa kuja kuwa mgeni rasmi kwenye hii hafla yenu nikiwa Mjumbe wa NEC", akasema M-NEC huyo.

M-NEC huyo aliwataka wale wanaokuwa wamefanikiwa kushinda kwenye uchaguzi kuhakikisha nao wanakuwa wanyenyekevu kwa waliowashinda, wasiwabeze badala yake wawaite na kuzungumza nao ili kumaliza tofauti zao kama zipo.

"Ukishinda mwite uliyemshinda, mzungumze ili kuondoa tofauti zeni zilizotokana na uchaguzi kama zipo, muulize, katika kugombea kwake alikuwa na malengo gani ya kukiendeleza chama, akikueleza mshirikishe katika kuyafanyia kazi hayo malengo", akasema M-NEC na kuongeza:

"Tunajua baadhi ya wagombea visirani vyao huwa haviishi haraka, sasa ikitokea uliyemshinda umemwita akakataa kujana mzungumze, basi tuletee taarifa sisi pale Wilayani, halafu tushughulike naye".

M-NEC huyo alionyesha kushangazwa kwake, kwamba kwa nini walioshindwa katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni hawakuweza kuhudhuria katika hafla kama hiyo iliyowahusu viongozi na wanachama kupongezana kwa kufanikisha uchaguzi.

"Hapa nadhani kuna jambo. au ninyi mnafikiaje, hamfiki ninavyofikiri mimi? kwani mnajisikiaje wale waliochukua fomu na hawakuja kwenye hafla hii, ina maana gani", alisema na kuhoji akimaanisha kulikuwa na tatizo linalotakiwa kufanyiwa kazi.

Katika hafla hiyo aliwaasa viongozi na wanachama wa CCM katika tawi hilo la Kibomu, kuongeza mashikamano, lakini pia kuhakikisha wanayatangaza yale yanayofanyika kwenye Kata yao katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Baadaye M-NEC huyo aliendesha amsha-amsha  kwa washiriki wa hafla hiyo kuchangia ujenzi wa Ofisi ya CCM ya tawi hilo, ambapo viongozi na wanachama kadhaa walijitokeza  kuchangia akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye ambaye aliahidi kwa njia ya simu kuchangia mifuko 10 ya saruji.

Baadaya asha-amsha hiyo ya kuchangia ujenzi wa Ofisi hiyo, sasa ikaingia zamu ya kila aliyehudhuria kupata chakula huku burudani ya muziki wa nyimbo za Chama Cha Mapinduzi ukihanikiza.

Safu ya juu ya viongozi wapya wa tawi hilo la Kibomu, mbali na Pili Busa ambaye ameshika tena nafasi ya Ukatibu wa   wengine na nafasi zao zikiwa kwenye mabano ni, Michael Mziray (Mwenyekiti), Elias John Komba (Mwenyekiti UVCCM), Abdul Rashid (Katibu UVCCM), Josephine Kombo (Mwenyekiti Wazazi), Omari Yahya (Katibu Wazazi), Lilian Nyamamanzawa (Mwenyekiti UWT) Swaumu Khalifa (Katibu UWT) na Godluck Rwejuma Katibu Mwenezi.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni Mussa Omari (mwenye fulana yakijani) akiwa na baadhi ya Viongozi wa CCM Tawi la Kibomu, Kata ya Kawe Wilayani Dar es Salaam, baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi katika hafla ya viongozi wapya na Wanachama wa CCM tawi hilo, kupongezana kwa kukamilisha vizuri Uchaguzi wa ndani ya Chama uliofanyika hivi karibuni katika tawi hiyo. Pamoja naye mwenye fulana nyeusi ni Mwenyekiti wa CCM wa Tawi hilo Michael Mziray.
Mgeni rasmi akiteta jambo na Mwenyekiti Mziray baada ya kufika meza kuu.
Mgeni rasmi akisaini Kitabu cha wageni baada ya kuketi meza kuu.
Katibu Mwenezi wa CCM Tawi hilo Godluck Rwejuma akitangaza kuanza hafla hiyo.
Katibu wa UWT wa tawi la CCM Kibomu Swaumu Khalifa akishangilia CCM baada ya kutambulishwa.
Katibu wa Wazaz wa tawi hilo Omari Yahya akisimama wakati akitambulishwa.
Mjumbe wa Shina Claudie Kimbe akishangilia "CCM Hoyee", wakati akitambulishwa.
"Wacha wasemee Chama Cha Mapinduzi kina wenyewe", akiimba kidogo wimbo wa CCM, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) tawi la Kibom Elias John Komba, wakati akitambulishwa. Elias ni mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Kikundi cha Tanzania One Thetre (TOT) cha CCM Marehemu Kapteni John Komba

Katibu wa CCM Tawi hilo la Kibomu akiendelea na utambusho wa viongozi kwa ngazi yake.
Pili Busa akishangiliwa baada ya kufanya utambulisho huo.
Kisha Pili Busa akasoma taarifa ya tawi hilo.
Baada ya kuisoma akamkabidhi mgeni rasmi.
Kisha zikafuatia shamrashamra.
Shamra shamra
Shamra shamra.
Mwenyekiti wa tawi hilo akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akizungumza na viongozi na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo. Chini ni viongozi na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi👇
👇
👇
👇
👇

Mgeni rasmi akizungumza na Viongozi wa Mashina ya CCM Kata ya Kibomu.
"Nawabariki kwa Jina la CCM, mkafanye kazi vizuri na kwa uadilifu kukijenga Chama", akasema Mwenyekiti Mstaa wa CCM tawi la Kibomu Mzee Raphael Mugabe, kuwabariki viongozi wapya wa tawi hilo ambalo yeye amestaafu baada ya kuongoza kwa miaka 17.
Mwenyekiti wa UVCCM wa tawi la Kibomu Elias John Komba akitangaza ahadi yake ya kuchangia ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi hilo.
Kisha akazungumza na Vijana walioalikwa kwenye hafla hiyo.
Katibu wa UVCCM Kata ya Kawe Kasim Ngonyani akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mgeni rasmi akiendesha amsha-amsha ya uchangiaji ujenzi wa Ofisi ya CCM Kibommu. Baadaye ikafuatia muda wa mlo, akitangulia mgeni rasmi👇
-mwisho-
© June 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages