LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 15, 2022

KISIWA CHA RUKUBA CHAONGEZA KASI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

Kisiwa cha Rukuba ni kati ya vijiji 3 vya Kata ya Etaro ya Jimbo la Musoma Vijijini.

Kisiwa hicho kina Zahanati ambayo sasa inapanuliwa kuwa Kituo cha Afya ambacho kitakuwa na Huduma za Afya zitakazotolewa hapo hapo Kisiwani badala ya wagonjwa na mama wajawazito kusafiri kwa mitumbwi kwenda kupata matibabu na huduma nyingine za Afya Musoma Mjini.

Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba wanaishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Rais wetu, Mhe Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapatia FEDHA za UJENZI wa Kituo chao cha Afya.

Serikali ilishawapatia Tsh MILIONI 250 na wiki hii watapokea tena Tsh MILIONI 250. Mchango wa Tsh MILIONI 500 kutoka Serikalini ni mkubwa na unashukuriwa sana sana!

Wakazi wa Kijiji cha Rukuba wanaendelea kuchangia NGUVUKAZI zao kwenye ujenzi huu.

Ustawi wa Kisiwa cha Rukuba unaendelea kuboreshwa na WAKAZI wa Kisiwa hicho kwa KUSHIRIKIANA vizuri sana na SERIKAL yetu.

Rukuba Shule ya Msingi
*Vyumba vya Madarasa vinatosha na vipo vya ziada viwili.
*Ofisi 2 za Walimu
*Maktaba ipo na vitabu vilinunuliwa na PCI (Tanzania) na Mbunge wa Jimbo 
*Madawati yapo ya kutosha na yalinunuliwa na Mbunge wa Jimbo.
*Nyumba za Walimu zipo za kutosha

Umemejua (solar) unaendelea kufungwa na Wakazi wa Kisiwani wanaomba  usambazaji uboreshwe.

Utunzaji wa Mazingira - mwezi uliopita Mbunge wa Jimbo aliwapatia MICHE 4,000 ya miti na matunda ya kupanda hapo Kisiwani.

Hoteli ya Kitalii iliyofungwa inaombwa ifunguliwe ili Kisiwa kianze tena kupata Watalii

PICHA zilizowekwa hapa zinaonesha:

*Picha 2 zinaonesha usafirishaji wa vifaa vya ujenzi kwa kutumia mitumbwi. Vifaa vinanunuliwa kutoka Musoma Mjini

*Picha 2 zinaonesha uezekaji wa Maabara ukiwa unakamilishwa

*Picha 3 zinaonesha kuanza kwa uezekaji wa Wodi ya Mama & Mdogo

OMBI KUTOKA KISIWANI RUKUBA

*Serikali inaombwa iwapatie Kivuko cha kusafirisha watu na bidhaa (k.m. samaki, mazao ya chakula) kati ya Ruhu (Wilaya ya Rorya), Kisiwa cha Rukuba na Mji wa Musoma (Wilaya ya Musoma). 

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alishawasilisha Serikalini ombi hilo (KIVUKO) na lile la BOTI ya PATROL/POLISI kwa ajili ya usalama wa wavuvi wetu na mali zao.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 15.6.2022











 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages