Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza majina ya Vijana waliomaliza kidato cha sita mwaka huu wa 2022 waliopangiwa kujiunga na Heshi hilo
Taarifa ya Jeshi hilo imesema waliochaguliwa aanatakuwa kuripoti kambini kuanzia Juni 3 hadi 17, mwaka huu katika kambi mbalimbali ikiwemo Kambi ya JKT Rwamkoma mkoani Mara, JKT Msange Tabora,JKT Ruvu Pwani,JKT Mpwapwa na Makutupora JKT Dodoma.
Mkuu wa Tawi la Utalawa kutoka Jeshi la Kujenga Taifa, Brigedia Jenerali, Hassan Mabena Mei 31,2022 jijini Dar es Salaam amesema, kambi nyingine vijana hao watakayo kwenda ni JKT Mafinga Iringa,JKT Mlale Ruvuma,JKT Mgambo,JKT Maramba mkoni Tanga,JKT Makuyuni Arusha, JKT Bulombora,JKT Kanembwa,JKT Mtabika mkoani Kigoma.
Ametaja kambi nyingine ni JKT Itaka Songwe,JKT Luwa,JKT Milundikwa Rukwa,JKT Nachingwea Lindi ,JKT Kibiti Pwani pamoja na Oljoro JKT Arusha. Kuona Majina Bofya Hapa
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇