Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali kesi ya msingi iliyofunguliwa na Wabunge 19 wa viti maalum Chadema akiwemo Halima Mdee na Ester Bulaya ya kupinga kuvuliwa uanachama na chama hicho.
Wabunge hao 19 waliwafukuzwa na Baraza Kuu la Chadema kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza hilo uliofanyika Mei 12, 2022, Mlimani City ambapo baada ya hapo Mdee wa wenzake walifungua kesi ya kupinga ambayo imetolewa uamuzi na Mahakama Kuu leo.
Mdee na wenzake waliingia Bungeni baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, ambapo Chadema ilijitokeza hadharani mara kadhaa kukanusha kuwa sio Wabunge wao na kwamba hawakuwasilisha majina ya Wabunge wao wa viti maalum.
Akizungumza leo nje ya Mahakama hiyo Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, wakili wa Chadema Peter Kibatala, amefafanua kuwa Mahakama pia imetupilia mbali maombi ya msingi ya kutaka kupewa kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama.
Aidha Kibatala ameeleza kuwa miongoni mwa sababu ya kutupiliwa mbali kwa maombi hayo ni kukosewa kwa jina la mjibu maombi namba moja ambaye ni Bodi ya Wadhamini ya Chadema iliyosajiliwa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika, ameomba sasa sheria kufuata mkondo wake, akisema kwamba kwa sasa hawaoni sababu ya Mdee wa wenzake kuendelea kusalia Bungeni.Halima Mdee akiwa na wenzake.
Your Ad Spot
Jun 22, 2022
Home
featured
siasa
HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAKWAA KISIKI LEO, MAHAKAMA KUU YAITUPA KESI YAO YA KUPINGA KUFUKUZWA CHADEMA
HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAKWAA KISIKI LEO, MAHAKAMA KUU YAITUPA KESI YAO YA KUPINGA KUFUKUZWA CHADEMA
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇