LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 13, 2022

TANZANIA NA JAMAICA ZAAHIDI KUONGEZA MAENEO YA USHIRIKIANO KATIKA UTALII

Na Mwandishi Maalumu, Dar es Salaam.

Serikali ya Tanzania na Jamaica zimeahidi kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji pamoja na elimu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina Smith katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

“Leo (jana) nimekutana na Mhe. Smith na tumejadili na kudhamiria kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji, elimu, uwezeshaji wa wanawake kiuchumi pamoja na vijana

Tanzania na Jamaica tumedhamiria kufanya kazi kwa karibu katika kutafuta njia bora ya kufungua fursa mpya kwa maslahi ya mataifa yote mawili,” alisema Balozi Mulamula

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina Smith amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Jamaica ambapo uhusiano huo umekuwa ni chachu ya maendeleo inayopelekea kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji na elimu.

“Ushirikiano uliopo baina ya mataifa yetu mawili umekuwa chachu ya maendeleo na lengo la ushirikiano huu ni kukuza, kuendeleza na kuimarisha uchumi wetu,” alisema Mhe. Smith

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa.  

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji, elimu, pamoja na afya. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica, Mhe. Kamina Smith katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages