Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mabenki Kenya Julius Alengo akimkabidhi Tuzo Mweka Hazina wa Benki ya NMB - Aziz Chacha ambaye alipokea tuzo ya Afisa Mtendaji Mkuu Bora Afrika kwa Mwaka 2022 (Tanzania) kwa niaba ya Ruth Zaipuna katika hafla iliyofanyika jijini Nairobi, Kenya.
CEO
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, mwishoni mwa wiki alitangazwa kuwa mshindi wa kipengele cha Afisa Mtendaji Mkuu Bora Africa kwa Mwaka 2022 (Tanzania) katika tuzo zilizoandaliwa na ‘African Bank 4.0 Summit – CEO Exclusive’ kipengele cha Benki na Uongozi wakati wa hafla iliyofanyika Ijumaa, Mei 27, 2022 katika hoteli ya Movenpick jijini Nairobi, Kenya.
Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Julias Alego - Mkurugenzi Mtendaji Tasisi ya Mabenki nchini Kenya na kupokelewa na Mweka Hazina Mkuu wa Benki ya NMB Aziz Chacha.
Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, Chacha alisema, “Ni heshima kubwa sana kwa Ruth Zaipuna kupokea Tuzo ya “African Banking CEO of the Year 2022 (Tanzania)”
Aidha, baada ya kupokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Ruth, Chacha alisema kuwa tuzo hiyo ameitoa kwa wafanyakazi wa NMB kwa kujitolea kwao na nia ya kuendelea kuwa mstari wa mbele wa vumbuzi, kuzingatia wateja, uthabiti, uaminifu, na usalama.
"Kwa maneno ya Ruth, natoa tuzo hii maalum kwa moja ya mtaji wetu mkubwa ambao ni wafanyakazi wa Benki ya NMB, wateja na wadau mbalimbali ambao bila wao, pengine tusingekuwa hapa tukisherehekea,” aliongeza.
Alibainisha kuwa benki yake kwa miaka mingi imekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia shughuli mbalimbali za kiuchumi katika sekta nyingi ikiwemo Utalii, elimu, kilimo, miradi ya kimkakati ya muda mrefu na afya.
"Ninatoa tuzo hii kwa wadau wa Benki ya NMB ambao wamejitolea kikamilifu katika azma yetu ya kubaki kweli bila kulinganishwa - benki imekuwa mstari wa mbele kwenye suala zima la ubunifu kwa kuzingatia wateja, uthabiti, uaminifu, usalama na usalama," aliongeza.
Mnamo Machi 2022, Ruth alitajwa kuwa miongoni mwa wanawake 74 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika katika sherehe za wanawake wanaofanya biashara kubwa barani Afrika na data zilizotumika kutengeneza orodha hiyo ilitolewa kutoka Bloomberg kulingana na taarifa iliyotolewa na Africa.com.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇