LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 21, 2022

RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA CHADEMA WAKIONGOZWA NA MBOWE, IKULU JIJINI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha majadiliano ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ikulu Chamwino Jijini Dodoma jana, Mei 20, 2022. Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho, na kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi baadhi ya waliohudhuria ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na Baadhi ya Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Baadhi ya Viongozi wa CCM pamoja na Serikali, Ikulu Chamwino baada ya mazungumzo yaliyofanyika jana, Mei 20, 2022. (Picha zote na Ikulu).

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages