**********************
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
Mei 8
MKUU wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallah ameeleza miradi 25 yenye thamani ya Bilioni 47.2 inapitiwa na Mwenge wa Uhuru kati ya miradi hiyo ni pamoja na kuweka jiwe la msingi mradi wa kipekee wa Ufugaji Afrika Mashariki na Ukanda wa Sahara .
Akipokea mbio za Mwenge wa Uhuru ukitokea wilaya ya Kibaha, huko Ruvu Darajani alieleza wilaya hiyo ina Halmashauri mbili ambapo Halmashauri ya Chalinze itatembelewa miradi 14 iliyogharimu milioni 937.8 na Bagamoyo miradi 11 yenye thamani ya Bilioni 46.3.
Aidha alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Bilioni 1.6 fedha za Uviko Chalinze na kujenga madarasa na miradi 66 ya shule za Sekondari .
Mkuu huyo wa wilaya alieleza kwamba, kwa Halmashauri ya Bagamoyo imepokea Bilioni 1.02 na kujenga shule shikizi 14 na Sekondari 37.
“Tunamuahidi Rais Samia kuwa hatutamuangusha ,katuteua kumsaidia kazi na hapa kwetu Chalinze na Bagamoyo tunapiga kazi ili kuleta maendeleo”alisema Zainab.
Zainab alifafanua, wilaya hiyo inategemea zaidi chanzo Cha mapato ya ndani Cha kokoto na mawe ambayo yanapelekwa jijini Dar es Salaam na maeneo jirani.
“Asilimia 60 ya mapato ya ndani yanatokana kwenye kokoto na mawe, ndio maana sisi miradi yetu ipo vizuri kwakuwa tunatumia malighafi inayotoka kwetu wenyewe “alisisitiza Zainab.
Vilevile akizungumzia suala la sensa ya watu na makazi alieleza, Zoezi la anwani na makazi wameshalitekeleza kwa asilimia 100 Hadi Sasa.
Mbunge Wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alisema ushauri, mapungufu wanayopatiwa watayafanyia kazi ili baadae miradi iwe Bora kwa maslahi mapana ya wananchi wa Chalinze.
Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Sahir Geraruma alihimiza usimamizi makini wa miradi kwani Serikali inatumia fedha nyingi hivyo inatarajia matokeo chanya yenye tija kwa Watanzania.
Miradi iliyopitiwa Chalinze ni pamoja na kuona shughuli za usafirishaji abiria -pikipiki ambao umegharimu milioni 41.8 kati ya fedha hiyo mil.32.6 Ni mkopo wa asilimia 4 ya vijana kutoka Halmashauri na milioni 9.2 Ni fedha ya wanakikundi na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la wodi ya mama na mtoto pamoja na upasuaji kwa fedha ya tozo.
Pia kuzindua mradi wa ukarabati wa barabara Pingo, kufungua vyumba viwili vya Madarasa na ugawaji wa vifaa vya ujenzi vinavyotokana na asilimia 5 ya mchango ya mwenge, kufungua kituo cha afya Sekondari Imperial, mradi wa kisima Kibiki na kuzindua ujenzi wa madarasa manne ya uviko19.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇