Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Newala mkoani Mtwara Aminata Mambiya jana alikuwa miongoni mwa Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali waliotunukiwa vyeti baada ya kuhitimu mafunzo katika Chuo cha Uongozi cha Magogoni, Jijini Dar es Salaam.
Aminata na Wahitimu wenzake walikabidhihiwa vyeti vyao na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi, katika Sherehe ya Mahafali ya Programu za Uongozi yaliyofanywa na Chuo hicho cha Uongozi kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Aalto (AEE) cha Finland, iliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
"Hakika najisikia faraja sana kupata mafunzo haya ya Uongozi. Kama inavyojulikana kwamba Uongozi ni kipaji, lakini vilevile viongozi wanatengenezwa, na kutengenezwa kwenyewe ni kwa njia kama hii ya mafunzo.
Japokuwa tayari mimi ni Kiongozi katika siasa kwa nafasi ya Katibu wa UWT Wilaya ya Newala na katika Taasisi yangu binafsi, lakini naamini elimu hii ya uongozi niliyopata itaniwezesha kutumikia kwa weledi zaidi nafasi zangu za uongozi nilizonazo na nyingine nitakazobahatika kupata baadaye", akasema Aminata.
Mbali na kuwa Katibu wa UWT Wilaya ya Newala, Aminata pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Shanghai Limited ambayo inajihusisha na kutoa elimu ya Lugha ya Kichina kwa kuwa yeye amesomea lugha hiyo nchini China.
Wengine waliopata vyeti hivyo pamoja na Aminata ni pamoja na Waziri Balozi Pindi Chana, Mkuu wa mkoa Mstaafu Paul Makonda, na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwengelo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi, akimkabidhi Cheti Katibu wa UWT Wilaya ya Newala Aminata Mambiya katika Sherehe ya Mahafali ya Programu za Uongozi yaliyofanywa na Chuo cha Uongozi kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Aalto (AEE) cha Finland, iliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam, jana.Aminata akipiga shoto kulia kwenda kupokea cheti chake kwa Naibu Waziri Ndejembi wakati wa Mahafali hayo.Kisha akapokea cheti chake kwa unyenyekevu mkubwa.Aminata akiondoka baada ya kupokea cheti chake.Aminata (kulia) akiwa na Wahitimu wenzake ambao pia walikabidhiwa vyeti.
Aminata (watatu kulia) akiwa na Wahitimu wenzake ambao pia walikabidhiwa vyeti.Aminata akiwa ameketi na wahitimu wenzake baada ya kupokea vyeti.
Aminata akiwa ameketi na wahitimu wenzake baada ya kupokea vyeti.Aminata akiwa ameketi na wahitimu wenzake baada ya kupokea vyeti.Aminata na wahitimu wenzake wakionyesha vyeti vyao katika tukio maalum la kupigiwa ala na Brasband ya Jeshi la Ulinzi la wamanchi wa Tanzania (JWTZ).
Aminata (kuahoto) na wahitimu wenzake wakionyesha vyeti vyao katika tukio maalum la kupigiwa ala na Brasband ya Jeshi la Ulinzi la wamanchi wa Tanzania (JWTZ).Picha ya pamoja ya Wahitimu, Naibu Waziri na Uongozi wa Chuo.Aminata akizungumza kidogo kwenye 'mike'
"Hongera sana mke wangu", akasema Joe Mambiya kumpongeza mkewe huku akimpatia maua kisha wakatabasamu wote."Hongera mhitimu mwenzangu", Mhitimu hiyo akamwambia aminata."Hongera Mzee" akasema mhitimu mmoja kumwambia Joe Mambiya ambaye ni Mume wa Aminata Mambiya.Marafiki wakimpongeza Aminata.
Aminata akiwa na mhitimu mwenzake katika picha ya kumbukumbu.Katibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Zena Ahmed Said akizungumza mwanzoni mwa sheherehe hiyo ya Mahafali.Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo hicho cha Uongozi akizungumza wakati wa Sherehe hiyo kuwapiga msasa wahitimu.Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi Dk. Laurean Ndumbao akizungumza kwenye sherehe hiyo ya Mahafali na kumkaribisha Mgeni rasmi kuzungumza na kugawa vyeti kwa wahitimu.Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi akizungumza na baadaye kukabidhi vyeti kwa wahitimu wakati wa Sherehe hiyo ya Mahafali ya Programu za Uongozi yaliyofanywa na Chuo cha Uongozi kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Aalto (AEE) cha Finland, iliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam, jana.
© May 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇