Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri ameshusha ushuru wa maliasili unaopaswa kulipiwa na wafanyabiashara na wabebaji wa mkaa wanaotumia bodaboda maarufu( WAKUBETI ),kutoka 37,500 Hadi 30,000 ili kupunguza utitiri wa tozo zinazowakabili na kuwasababishia kukwepa ushuru kwa kupita njia za panya.
Hatua hiyo imekuja kufuatia Wakala wa Misitu TFS Kibaha kuingia katika msuguano na wafanyabiashara hao ambao wamesusia kupita getini na kuamua kupita vichochoroni kukwepa ushuru ndani ya mwezi mmoja Sasa.
Akiingilia kati mgogoro huo, huko Kwala baada ya wafanyabiashara wa mkaa kugomea ushuru mpya ya sh.37,500 kutoka ushuru wa zamani ya 25,000, Msafiri amelazimika kutoa maagizo manne yanayolenga kujenga mahusiano baina ya pande hizo mbili.
Agizo jingine Ni kuvunja uongozi uliopo wa wafanyabiashara wa mkaa kwa like alichodai umekiuka sheria kwa Kuwa miongoni mwa wanaofanya vurugu na kuisababishia hasara Serikali kutokana na kugomea kulipa ushuru wa Serikali.
Msafiri ametoa tamko kuanzia sasa kituo kikuu Cha kuuzia mkaa Ni Mlandizi badala ya kuhangaika na pikipiki kwenye barabara kukimbilia soko Mbezi na kwingine.
Awali ,Wakubeti akiwemo Hosea Paulo na Yasin Rajabu wameeleza ,licha ya hayo bei ya shamba nayo ni kubwa 90,000 wakati zamani walilipia 60,000 .
Akijibu hoja hizo Meneja wa TFS Kibaha ,Mukama Kusaga Amefafanua, kwa mujibu wa sheria ya misitu na.14 ya mwaka 2002 na kanuni zake mfanyabiashara wa mkaa anatakiwa kulipa sh.250 kwa kila kilo ya mkaa au 12,500 kwa gunia lenye kilo 50.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇