Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama anatarajia kuzindua ugawaji wa hatimiliki ardhi za kimila zaidi ya 2600 na uwekaji wa mawe ya msingi katika ujenzi wa majengo ya masijala katika vijiji vya Makanda na Msisi wilayani Bahi, mkoani Dodoma kesho Jumamosi Aprili 30, 2022.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu, Habari na Mawasiliano kwa Umma wa Mpango wa Kurasimisha Raisilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Gloria Mbilimonyo akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Masijala la kuhifadhia nyaraka zikiwemo hatimiliki za ardhi za kimila katika Kijiji cha Msisi, Bahi mkoani Dodoma.
Ujenzi wa jengo la masijala ukiendelea katika Kijiji cha Makanda |
Mwenyekiti wa Kijiji cha Makanda akifungua mkutano kwa ajili mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu namna ya kutumia hatimiliki za ardhi za kimila kupata mkopo benki na taasisi zingine na fedha.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇