Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limekubali kuwa msimamizi wa uchaguzi wa viongozi wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) unaofanyika Jumamosi Aprili 9, 2022 kwenye ukumbi wa Splended, Ilala Bungoni Dar esa Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa SHIWATA, Michael Kagondela alisema Kamati ya kusimamia uchaguzi imekalisha maandalizi na BASATA ndio wakataosimamia uchaguzi huo ambao utamchagua Mwenyekiti na wajumbe 15 wa Bodi.
Kagondela aliwataja waliochukua fomu na kurejesha ni Deogratius Kway pekee aliyechukua fomu ya kugombea Uenyekiti.
Wajumbe ni Wasanii wawili maarufu wa filamu nchini Ahmed Olotu (Mzee Chilo) na Lomole Matovolwa (Big) na mfanyabiasha maarufu wa vifaa vya michezo nchini Abbas Issere.
Wengine ni mwandishi mkongwe nchini Peter Mwenda na mpiga picha mkongwe wa TBC, Suleiman Kissoky.Wengine ni mwanamuziki maarufu wa Bendi ya Hisia Sound, Asha Salvador pia yumo mcheza netiboli wa zamani wa timu ya taifamkugunzi na kiongozi wa Chama cha Netiboli nchini (CHANETA), Mwajuma Kisengo,
Wengine ni kiongozi wa Chama cha wacheza sarakasi nchini, Suleiman Pembe, Christian Hall, Anna Katikiro, Charles Kihiyo, Elizabeth Magwaja, John Mabula na Hassan Mambo.
Viongozi watakaochaguliwa watakaa madarakani kwa miaka mitatu kabla ya kufanya uchaguzi mwingine.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇