Bunge, Dodoma
Mwili wa aliyekuwa Mbuge wa Viti Maalum mkoa wa Rukwa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Marehemu Irene Ndyamkama utapelekwa aliyefariki Dunia jana katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha mkoa wa pwani, utaagwa Bungeni Jijini Dodoma, keshokutwa, Jumatano, Aprili 27, 2022.
Taarifa ya Bunge imesema, ratiba hiyo imefikiwa katika Kikao cha pamoja baina ya Tume ya Utumishiwa Bunge na Kamati ya Uongozi ya Bunge kilichofanyika leo na kukubaliana mwili ufikishe Bungeni Jijini Dodoma siku hiyo kwa ajili ya Ibada Maalum na Waheshimiwa Wabunge kutoa heshima zao za mwisho.
"Pia Uamuzi huo umefikiwa baada ya Uongozi wa Bunge kushauriana na kukubaliana na familia ya Marehemu Irene", imesema taarifa hiyo ya Bunge.
Taarifa imeongeza kuwa baada ya Wabunge kutoa heshima zao za mwisho,mwili wa wamarehemu utapelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, kusubiri kusafirishwa siku ya Alhamisi 28 Aprili 28, 2022 kupelekwa Sumbawanga, Mkoani Rukwa ambapo kutakuwa na shughuli ya kuaga mwili wa marehemu kwa utaratibu utakaoandaliwa na uongozi wa Serikalina Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani hapo.
"Mheshimiwa Irene Alex Ndyamkama aliyefariki siku ya Jumapili, Aprili 24, 2022 katika Hospitali ya Tumbi Mkoa wa Pwani inatarajiwa atazikwa Aprili 29, 2022 Mpanda, Mkoani Katavi.
Ofisiya Bunge inaendelea kuratibu taratibu za mazishi kwa kushirikiana na familia yaMarehemu, taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema peponi", imesema taarifa hiyo ya Bunge. Irene Alex Ndyamkama
Your Ad Spot
Apr 25, 2022
Home
featured
KIJAMII
MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA VITI MAALUM (CCM) MKOA WA RUKWA IRENE NDYAMKAMA, KUAGWA BUNGENI KESHOKUTWA
MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA VITI MAALUM (CCM) MKOA WA RUKWA IRENE NDYAMKAMA, KUAGWA BUNGENI KESHOKUTWA
Tags
featured#
KIJAMII#
Share This
About Bashir Nkoromo
KIJAMII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇