Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wamemchagua kwa asilimia 100 Katibu Mkuu wa Mstaafu wa CCM Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM baada ya kupata kura 1875 za ndiyo zikiwa zote ndizo zilizopigwa.
Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa ameshinda kwa kishindo, Kinana alimshukuru Mwenyekiti wa CCM Rais samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumpa heshima kupitia vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ambavyo yeye (Samia) aliviongoza.
“Juzi uliniita nikawa najiuliza nimeitiwa nini, nikajua ni katika kusalimiana. Rais akaniambia nataka uwe Makamu Mwenyekiti, nikamwambia sina hiari, sina budi kukubali, napenda kukuhakikishia Mwenyekiti nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kufikia matarajio yako, Niseme sitokuangusha”, akasema Kinana.
Pia Kinana amewashukuru Wajumbea wa Kamati Kuu ya CCM kupitisha jina lake, sanjari na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kwa kupitisha na kumuidhinisha kugombea nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti wa CCM.
“Mmenipa imani kubwa, na mimi nitakitumikia Chama changu, wana CCM na Watanzania kwa umahiri mkubwa na wala siyo kwa utukufu uliotukuka”, akasema Kinana.
Pia amemshukuru Makamu Mwenyekiti Mstaafu Mzee Philip Mangula akisema kuwa amejifunza mengi kutoka kwake na kumpongeza kwa kustaafu kwa heshima, kwa kuwa Kama asingeamua kustaafu, basi asingekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM.
Makamu Mwenyekiti Kinana aliwashukuru Wenyekiti wote waliotangulia tangu Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere hadi wa sasa Rais Samia Suluhu Hassan na Wanachama wote wa CCM kwa kumuona kuwa anasifa za kuwa kiongozi wa nafasi aliyopata huku akisisitiza kuwa sifa hizo alizopata ni za viongozi na wana CCM hao na siyo za kwake.
" Wenyekiti wote waliotangulia tangu Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere hadi wa sasa Rais Samia na Wanachama wote wa CCM kwa kuniona kuwa nizo sifa za kuwa kiongozi wa nafasi hii, lakini nasema kwamba sifa hizo siyo zangu bali ni za Viongozi na Wana CCM wote, isipokuwa mapungufu ni yangu", alisema Kinana.
Kinana amesema, kazi yake ya kwanza ni kwenda kukisimamia Chama ili kiendelee kuwa imara na kwamba ili kiwe imara ni lazima Demokrasia itamalaki ndani ya Chama kwa maana ya kila mwanachama kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa bila upendeleo.
“Lazima wanachama wawe huru kutoa mawazo, hakuna mwenye hakimiliki ya mawazo, lazima tumsikilize kila mwananchi, na wanachama wakimchagua mtu kwani sisi ni nani wa kupinga.
“Nimekuwa nikimsikia Rais akisisitiza mara zote katika kusimamia haki, nilimsikia akisema Vyeti peke yake siyo sifa, Vyeti viende na uadilifu, kukubalika, Nchi hii inajulikana kwa Haki ndani na nje ya Nchi”, akasema Kinana.
Alisema kimsingi CCM si mali ya Serikali ila Serikali zinatokana na CCM ambapo alieleza kuwa CCM haipokei maelekezo kutoka Serikalini.
“CCM haiagizwi na Serikali, CCM ndiyo inayoiagiza Serikali, na wanaokwenda kuomba kura ni CCM sio Serikali, nina wasihi Viongozi wetu msitudhulumu hiyo haki”, akasema Kinana.
“Siyo vizuri kuisema vibaya Serikali, lakini ni lazima CCM tuiseme pale tunapoona naifanyi sawa, ispokuwa hatutaisemea kwa kukejeli, tutaitana kwenye Vikao vyetu vya ndani, si sawa kwa Mwana CCM kwenda hadharani kuisema vibaya Serikali yake”, akabainisha Kinana.
Kinana alisisitiza, Chama cha Mapinduzi ni kikubwa na kinakubalika hivyo ni lazima CCM ibaki kuwa masikio ya Wananchi
“Hili nalo ni la umhimu, nataka niwasihi, hakuna chama cha mtu, kuna Chama cha Mapinduzi, hivyo ndani ya hiki chama hakuna ukanda, haya mambo ya ukanda, ukabila, udini tukae nayo mbali.
Maama kuna mtu mwingine akikosa hoja na maarifa anaingia kwenye kichaka cha udini, ukabila, ubara na Uzanzibar. hiyo si sawa kwa chama hiki, tunaweza kutofautiana kwa sababu nyingi lakini siyo kikanda au kikabila”, aonya Kinana.
![]() | |
| Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Samia Suluhu Hassan akipiga kura kwa
ajili ya kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana
katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya
Kikwete Jijini Dodoma leo. Zifuatazo ni matukio mbalimbali ya Mkutano huo. tafadhali zitazame👇 |
M










No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇