Florida, Marekani
Bibi Harusi Danya Svoboda ameingia matatani pamoja na Mhudumu wake Joycelyn Bryan, baada ya kudaiwa kuweka bangi katika chakulana kusababisha wageni waalikwa kwenye Sherehe ya harusi yake waliokula chakula hicho kulewa hadi baadhi yao kupoteza fahamu.
Mitandao ya Kijamii, imeripoti kuwa baada ya tukio hilo kugundulika ilibidi Maofisa wa Polisi kuitwa na kufika kwenye sherehe ya harusi hiyo kusaidia wageni waalikwa ambao walikuwa wanahisi kama wamelishwa dawa za kulevya hadi baadhi yao kupoteza fahamu.
"Baada ya kula chakula nilianza kujisikia kama mlevi hivi..., nilipomuuliza bibi harusi kama waliongeza kilevi chochote katika chakula, akajibu ndiyo, tuliongeza bangi, kisha akatabasamu", alisema mmoja wa wageni waalikwa katika harusi hiyo alitoa ushahidi kwa maofisa wa Polisi.
Baada ya polisi kufanya vipimo kwenye vyakula na vinywaji vya sherehe ya harusi hiyo, vyakula vilibainika kuwa na chembechembe za bangi, ndipo Bibi Harusi na mhudumu wake huyo wakakamtwa na kufunguliwa mashitaka ya kufanya maamuzi ya kizembe na kuwalisha watu bangi bila ridhaa yao.
Katika Jimbo la Florida inasemekana bangi ni halali kama ikitumika kimatibabu, lakini si kwa matumizi ya burudani tofauti na katika baadhi ya majimbo nchini Marekani.Bibi Harusi huyo akikata keki na Mumewe
Your Ad Spot
Apr 24, 2022
Home
featured
KIJAMII
BIBI HARUSI MATATANI KWA KUWEKA BANGI KATIKA CHAKULA, WAGENI WAALIKWA WALEWA CHAKARI NA WENGINE KUZIMIA
BIBI HARUSI MATATANI KWA KUWEKA BANGI KATIKA CHAKULA, WAGENI WAALIKWA WALEWA CHAKARI NA WENGINE KUZIMIA
Tags
featured#
KIJAMII#
Share This
About Bashir Nkoromo
KIJAMII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇