Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) - Bara Abdurahman Kinana leo anaendelea na ziara yake ya kwanza ya mikoani kukagua uhai na kuimarisha Chama, tangu alipochaguliwa kwa kura asilimia 100 za wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika Aprili Mosi, 2022 Jijini Dodoma.
Katika ziara hiyo ambayo aliianzia jana katika mkoa wa Pwani, na kuonyesha msisimko mkubwa kwa WanaCCM na wananchi kwa jumla kuonyesha ari ya kumpokea kwa shangwe, nderemo na vifijo, leo Jumatatu, Aprili 25, 2022, Kinana ataendelea na ziara hiyoa katika mkoa wa Tanga.
Akiwa mkoani Tanga, Kinana anatarajiwa kuzungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali na kufanya shughuli nyingine za kuimarisha Chama kulingana na ratiba atakayokuwa amepangiwa na wenyeji wake.Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) - Bara Ndugu Abdurahman Kinana
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇