WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka nchini kwenda Qatar na Jordan kwa ziara ya kikazi.
Akiwa huko, Waziri Mkuu atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika vikao na viongozi wakuu wa nchi hizo.
Tanzania na Qatar zimepanga kuanzisha Tume ya Ushirikiano ya Pamoja ambayo itasimamia masuala mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo na usafiri wa anga.
Akiwa Jordan, Waziri Mkuu atashiriki mkutano wa kujadili usalama katika eneo la Kusini Mashariki mwa Afrika hususan Msumbiji na maeneo jirani. Mkutano huo wa Aqaba Process on East Africa, utafanyika Machi 24, 2022 katika mji wa Aqaba, Jordan.
Mkutano huo ambao umeitishwa na Mfalme wa Jordan, Mheshimiwa Abdulla wa II ni wa tatu kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015 na huwakutanisha viongozi wakuu wa nchi za ukanda wa Mashariki ya Afrika ili kujadili changamoto za ugaidi na namna ya kudhibiti.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇