Hayo yamesemwa leo Machi 4, 2022 na Mwenyekiti Kamati wa Kamati ya Wanawake Taasisi ya Mifupa MOI, Salma Amani alisema mapato ya mradi huo yatawawezesha Kamati ya Wanawake ya TUGHE kutoa huduma za mikopo ya riba nafuu kwa wanawake wote wa MOI hasa wanachama hai.
"Tunatamani Sana kupatiwa nafasi, japo tukaendesha mradi wa duka utakaosimamiwa na wanawake." alisema Bi. Salma.
Bi. Salma aliomba uongozi wa MOI kufuatilia fursa zinazotolewa na Rais Samia Suluhu Hasan za kuwapatia mikopo watumishi wa Umma ili kuwaongezea kipato pia alizidi kuwaomba wamama hao kwaumoja kuendele kumuunga mkono Rais mwanamama. Samia Hassan Suluhu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kutambua na kuthami mchango wa watumishi hasa wanawake kama chachu ya maendeleo endelevu kwa Taifa letu kwa kufanya kazi kwa bidii.
Pia Wamama Tawi la TUGHE MOI tuna mpongeza Waziri wa Afya Dada yetu kipenzi Ummy Mwalimu kwa kuteuliwa kwake na iwe chachu kwa kuona umuhumu wa sisi wanawake kwa kujitokeza wa wingi kugombea nafasi mbalimbali.
Bi. Salma amewaomba Wanawake zaidi wajitokeze kujiunga na TUGHE ili waweze kupiga hatua katika maendeleo.
Wanawake wa TUGHE kupitia Chama hicho waliwatembelea watoto waliolazwa wodini katika Taasisi hiyo nakutoa msaada wa vitu mbalimbali kiwemo baiskeli ya kutembele kwa mtoto aliyepoteza uwezo wa kutembea na kuwatembele wanawake wenzao waliofungwa Geraza la Ukonga na kuwapa faraja. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mwenyekiti Kamati za Wanawake, TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Baraza Kuu TUGHE Taifa Georgina Chirwa akizungumza jambo katika Kongamano la Maadhimisho Siku ya Wanawake Ulimwenguni leo Machi 4, 2022 kwenye Ukumbi wa Taasisi ya Mifupa MOI ambapo Kilele cha Maadhimisho haya kila Mwaka Duniani hufanyika Machi 8.
Wamama wakishangilia mara Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Taasisi ya Mifupa MOI Salma Amani alipokua akisoma hutuba katika Kongamano la Maadhimisho Siku ya Wanawake Ulimwenguni leo Machi 4, 2022 kwenye Ukumbi wa Taasisi ya Mifupa MOI.
Mshereheshaji katika Kongamano la Maadhimisho Siku ya Wanawake Ulimwenguni leo Machi 4, 2022 kwenye Ukumbi wa Taasisi ya Mifupa MOI. Zaituni Bembe akizungumza jambo kabla ya kukaribishwa Mwenyekiti Kamati za Wanawake, TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Baraza Kuu TUGHE Taifa Georgina Chirwa ili amkaribishe Katibu TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Baraza Kuu TUGHE Taifa Sara Rwezaura.
Katibu TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Baraza Kuu TUGHE Taifa Sara Rwezaura. Ninafuraha ya ajabu kuona wamama mkiwa na nyuso za furaha na mnavyo shirikiana kwa umoja wenu na mnajitoa kwa kujichanga nakusaidia wamama wenzetu mkiongozwa na Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Taasisi ya Mifupa MOI Salma Amani Mungu awabariki sana na mzidi kuwa wamoja.
Mkurugenzi wa Tiba Taasisi ya Mifupa MOI Dkt. Samwel Swai akisalimia Wamama katika Kongamano la Maadhimisho Siku ya Wanawake Ulimwenguni leo Machi 4, 2022 kwenye Ukumbi wa Taasisi ya hiyo.
Mkurugenzi wa Tiba Taasisi ya Mifupa MOI Dkt. Samwel Swai akizungumza na Wamama katika Kongamano la Maadhimisho Siku ya Wanawake leo Machi 4, 2022 kwenye Ukumbi wa Taasisi ya hiyo na kuipongeza Kamati nzima ya maandalizi na wamama wote walioshiriki kuandaa Kongamano la Maadhimisho Siku ya Wanawake na kama Taasisi itatoa ushikiano na kuhakikisha mnafanikiwa malengo yeu kwani ninyi ni Jeshi kubwa na mkizingatia tunaye Mama yetu Rais Samia Suluhu Hasan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu hivyo lazima tukubari kuendana na kasi katika kufanya kazi kwa bidii na kuleta maendeleo.
Mwenyekiti Kamati za Wanawake, TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Baraza Kuu TUGHE Taifa Georgina Chirwa akimpatia zawdi mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya MOI wakati wa Kongamano la Maadhimisho Siku ya Wanawake Ulimwenguni leo Machi 4, 2022.
Wamama wakiwa katika Kongamano la Maadhimisho Siku ya Wanawake Tawi la TUGHE MOI leo Machi 4, 2022.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇